EACOP YAPONGEZWA KULINDA MAZINGIRA YA MWAMBAO WA TANGA - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Wednesday, October 16, 2024

EACOP YAPONGEZWA KULINDA MAZINGIRA YA MWAMBAO WA TANGA

Washiriki katika warsha ya siku mbili ya EACOP wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya majadiliano ya urejeshwaji wa mazingira ya asili ya bahari sambamba na ajira wa wakazi katika pwani ya Chongoleani mkoani Tanga.


NA MWANDISHI WETU

MRADI wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika ya Mashariki (EACOP),  umesifiwa kwa kurejesha vizuri mazingira ya asili ya viumbe hai wa baharini, kupanda mikoko na kuotesha mwani katika mwambao wa Mkoa wa Tanga.  EACOP inashirikiana na taasisi 10 katika zoezi hili kwa sababu inajenga temino  kwenye Ras ya Chongoleani kwa ajili ya kuhifadhi mafuta ghafi kwa ajili ya masoko ya kimataifa.


Akizungumza jana baada ya warsha ya siku mbili  ya kurejesha mazingira ya asili ya baharini na kurejesha ajira zinazohusiana na bahari iliyoandaliwa na EACOP Jijini hapa, Ofisa Uvuvi wa Mkoa wa Tanga,


 Gladys Manyika, aliishukuru EACOP kwa mradi wa urejeshwaji wa mazingira ya asili ya bahari, na kusema kwamba sasa ni dhahiri kwamba mradi hautaadhiri shughuli za uvuvi bali utakuwa na tija kwa wavuni, kwani  mradi ukifikia mahali pazuri itapelekea kuongezeka kwa wingi wa samaki.


“Utekelezaji wa mradi huu mpaka sasa una miaka mitatu. Sasa tuna sababu za kuridhika kwamba mradi hautaathiri shughuli za uvuvi.  Aidha maafisa wa EACOP  wanakutana na wavuvi mara kwa mara ili kujenga uwelewa wa mradi huu.”


Kiongozi wa nyasibandia, kutoka Shule Kuu ya Sayansi na Teknolojia ya Uvuvi, Dkt Blandina Lugendo, amesema zoezi la kulinda bahari katika mwambao wa Tanga linaendelea.  “Sisi ni wadau katika programu hii.  Mradi wetu unaendelea na ni salama kabisa. Nyasi zitavutia samaki wengi kuishi katika eneo hilo na hili litakuwa na jita kwa wavuvi.”


Dkt Lugendo aliwatoa hofu wananchi kwa kusema eneo lililoathirika na mradi na mradi ni dogo wakati eneo linalopandwa nyasi hizo ni kubwa zaidi.


“Mradi huu ukikamilika utaongeza idadi ya Samaki majini kwani mazalia ya Samaki yatakuwa yameongezeka na itakuwa  ni faida kwa wananchi na wavuvi wa eneo hilo la Chongoleani,” alisisitiza.


Mapema Mshauri ya Sayansi ya Baharini wa EACOP (Scientific Marine Advisor) Bw Matthew Richmond, alieleza kuridhishwa na kazi inayotekelezwa na EACOP ni kutokana na utafiti mkubwa uliofanywa kuhusiana na nmanma bora ya urejeshwaji wa uoto wa asili wa bahari.


“Hayo yote yanafanywa katika jitihada za kutunza mazingira ya Bahari na viumbe hai vya bahari ilikuendelea kuwa na tija kwa watumiaji wote wa Bahari,” alisema Bw Richmond.


EACOP ina programu ya kulinda mazingira kutokana na shughuli za mradi ambayo inatekelezwa na taasisi 10.


Alieleza kwamba programu ya kulinda mazingira  ya habari itaendelea pengine kwa miaka 20 au 30 au zaidi katika eneo hilo. “Hii itategemea tafiti zinazofanywa wakati huu na za baadaye,” alisema na kuongeza kuwa kazi iliyokwishafanywa itailetea sifa serikali ya Tanzania duniani kwa kulinda vizuri mazingira.


Aidha, aliongeza, miradi inayotekelezwa inatoa ajira kwa Watanzania na ujuzi wa kisasa wa kulinda mazingira ya bahari.


Baadhi ya wadau wakifuatilia kwa makini wasilisho la EACOP kwenye warsha ya siku mbili iliyofanyika jijini Dar es Salaam, lengo ikiwa ni kujadili  maendeleo ya mradi sambamba na  namna bora ya urejeshwaji wa uoto wa asili  katika mwambao wa pwani ya Chongoleani mkoani Tanga

No comments:

Post a Comment