NA MAGENDELA HAMISI
SHIRIKA la Foundation For Civil Society (FCS) na Baraza la Ushauri la Watumiaji Huduma za Usafiri Ardhini (LATRA CCC) wameingia makubaliano kwa miaka mitatu kwa lengo la kuongeza ufanisi na kufikia malengo mahusis ya baraza hilo.
Shughuli ya kusaini makubaliano hayo yamefanyika leo Oktoba 22 jijini Dar es Salaam mbele ya waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari.
Awali kabla ya kutiliana saini mkataba huo wa miaka mitatu, Mkurugenzi Mtendaji wa FCS, Justice Rutenge amesema kwamba huo ni sehemu ya mikakati yao kuhakikisha wanashirikiana na taasisi mbalimbali ili kuleta matokeo chanya kwa taifa.
"Miezi kadhaa iliyopita tuliingia makubaliano na Baraza la Ushauri la watumiaji wa huduma za mawasiliano (TCRA CCC) na leo tunaingia mkataba mwingine na LATRA CCC, na lengo ni moja tu, kufanikisha baraza ili kufiikia malengo yake," amesema.
Ameongeza kuwa anaamini kushirikiano kwao kutaongeza tija kwa maana shughuli zinazofanywa na baraza hilo ni kama uti wa mgongo kwa taifa kwani usimamizi madhubuti wa usafiri wa ardhini unawezesha kuinua uchumi kwa kufanikisha biashara kuingia sokoni na viwandani kwa wakati.
"Bila usafiri thabiti wa ardhini bidhaa haziwezi kutoka viwandani kwenda sokoni, hivyo ushirikiano wetu, utareta tija stahiki," amesema
Pia amesema, usafiri ni kiungo muhimu katika utoaji wa huduma za maendeleo, kwa
ujumla tunaweza kusema bila miundombinu ya usafiri imara inakua vigumu sana kwa taifa kufikia malengo ya maendeleo endelevu, LATRA CCC ni sehemu muhimu katika kuhakikishwa miundombinu inaimarishwa na inatumiwa vyema kwa manufaa ya kila mtanzania hasa wanaotumia biashara na usafirishaji katika maisha yao.
Naye Katibu Mkuu wa LATRA CCC, Daud Daud amesema kuwa Ushirikiano huo umelenga kufanya miradi ya pamoja katika kuongeza uwezo wa kiutendaji ili kutoa huduma bora kwa watumiaji wa usafiri wa ardhini.
"Mradi huu tunautekeleza hasa katika maeneo makubwa mawili ,eneo la kwanza ni kutengeneza miradi kwa pamoja na kutekeleza kwa pamoja, eneo la pili ni kutoa elimu kwa watumiaji wa huduma za usafiri wa ardhini, pamoja na kujiongezea uwezo sisi watendaji ili kutoa huduma inayoendana na wakati" amesema.
Pia hakusita kutoa wito kwa wakandarasi bao wamepewa jukumu la kujenga Barbara nchi hususan jijini Dar es Salaam kuharakisha ujenzi ili kuleta matokeo chanya kwa nchi.
"Naipongeza Serikali yetu inayoongozwa na Rais wetu mpendwa Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuona umuhimu wa kuendeleza miradi ya Barabara nchi na kutoa fedha za kutosha kufanikisha hilo," amesema





No comments:
Post a Comment