NA MAGENDELA HAMISI
WITO umetolewa kwa jamii kutoa nafasi kwa wasichana kushika nafasi za uongozi kwa kuwa wanauwezo kuleta mabaadiliko chanya na kuchangia maendeleo ya nchi.
Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es Salaam na Jane Sembuche ambaye ni Mkurugenzi Mkazi wa Plan International wakati akihitimisha Kampeni ya Chukua Hatamu 'Girls Takeover' ambapo wasichana zaidi ya 40 wameshiriki katika hafla hiyo.
Kampeni hiyo, inatekelezwa na shirika hilo ikishirikiana na Serikali lengo likiwa ni kuhakikisha mtoto wa kike anatimiza ndoto zake ikiwa atapatiwa fursa ya uongozi katika nyanja mbalimbali ikiwemo kwenye siasa.
"Shughuli ya namna hii, tunaifanya kila mwaka Oktoba 11na na inakwenda pamoja na kuheherekewa siku ya mtoto wa kike duniani kote na tunaiita 'Girls Takeover' kwa tafsiri ya Chukua Hatamu ambayo ni mahususi kumhamasisha msichana kufanya jitihada na kujituma pindi anapopewa nafasi ya uongozi Kwa maana tunaamini anaweza," amesema
Ameongeza kuwa Kwa namna wasichana wanavyokuwa na ujasiri ikiwa watahamasishwa wataweza kuwa viongozi wazuri na kuleta maendeleo stahiki katika jamii na mifano iko mingi na ya kuigwa kwa jinsi hiyo kufanya vema na kinachotakiwa na kuwapa hamasa kuwa wanaweza.
Akizungumzia uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba mwaka huu Mkurugenzi huyo Mkazi wa Plan International Tanzania amesema kuwa pamoja na shirika hilo kutekeleza Kampeni ya Girls takeover lakini pia lina kampeni nyingine ya "Sikia Sauti zetu " ili kuwezesha sauti za wasichana sehemu mbalimbali wanahamasika kuzungumza nakuleta changamoto zao katika sehemu husika.





No comments:
Post a Comment