MBUNGE WA BUSANDA AHIMIZA WAJASIRIAMALI KURASIMISHA BIASHARA - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Tuesday, October 8, 2024

MBUNGE WA BUSANDA AHIMIZA WAJASIRIAMALI KURASIMISHA BIASHARA

 


NA MWANDISHI WETU

MBUNGE wa Jimbo la Busanda , Tumaini Brygeson Magessa amewataka wajasiriamali wanaoshiriki katika maonesho ya  7 ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini katika viwanja vya EPZA Bombambili mkoa wa Geita kutumia fursa hiyo kurasimisha biashara zao  ili ziweze kukua.

 

Magessa ametoa rai hiyo, Oktoba 07, 2024 wakati alipotembelea banda la Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) lililopo  katika viwanja vya EPZA Bombambili mkoa wa Geita na kupata huduma ya usajili wa papo kwa papo.


Akionesha kuridhishwa na huduma zinazotolewa bandani hapo Mhe.Magessa ametoa wito kwa BRELA na wadau wengine wanaotoa huduma katika maonesho kuhakikisha  wajasiriamali mbalimbali wanakua, hivyo wasaidiwe kwa kupatiwa huduma na elimu ili waweze kurasimisha biashara zao.  


Pia ameipongeza BRELA kwa huduma nzuri za utoaji wa elimu pamoja na huduma ya sajili mbalimbali inazozitoa  kwa kuwa  zitawawezesha wafanyabiashara wadogo, wa katı na wakubwa waliojitokeza katika maonesho haya kupata huduma stahiki za urasimishaji wa biashara zao kwa urahisi.


Maonesho ya 7 ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini  yaliyoanza tarehe 2 Oktoba,2024 yamefunguliwa rasmi  tarehe 5 Oktoba na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe.Dotto Biteko yatahitimishwa  tarehe 13 Oktoba, 2024 katika viwanja vya EPZA Bombambili mkoa wa Geita, kauli  mbiu  ya maonesho haya  ni "Matumizi ya Teknolojia na Nishati Safi katıka Sekta ya Madini kwa Maendeleo Endelevu”.

No comments:

Post a Comment