MTUMBUKA ASHINDA KURA ZA MAONI KITONGOJI CHA KAZOLE MJINI - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Thursday, October 24, 2024

MTUMBUKA ASHINDA KURA ZA MAONI KITONGOJI CHA KAZOLE MJINI


Mshindi wa kura za maoni kwa nafasi uenyekiti wa Kitongoji Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Said Mtambuka mwenye fulana ya CCM, waliokaa chini akiwa na baadhi ya wajumbe katika Shina namba 5, Kazole Mjini kata ya Vikundi mkoani Pwani wakifurahia ushindi huo.

NA JUMANNE AMBALI, PWANI

SAID Mtumbuka amefanikiwa kutwaa nafasi ya kukiwakilisha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwania nafasi ya uenyekiti wa kitongoji cha Kazole Mjini, Kata ya Vikindu mkoani Pwani.


Mteule huyo wa nafasi ya uenyekiti wa kitongoji alifanikiwa kutwaa nafasi hiyo baada ya kushinda aliyekuwa akitetea nafasi hiyo, Cathibert Mwaya kwa kura 151 kati 285 zilizopigwa.


Kwa mujibu wa mtoa habari wetu, amesema kwamba uchaguzi wa kura za maoni za CCM katika kitongoji hicho zilifanyika jana Oktoba 23 na kutokana kura kugongana kwa wagombea wawili ukaamliwa  kurudiwa leo Oktoba 24, 2024.


"Uchaguzi ulifanyika jana na wagombea wawili ambao ni Mwaya aliyekuwa akitetea nafasi yake alifungana kura kwa kila mmoja kupata alama 91 na mgombea mwingine akipata kura 5," amesema.


Amesema baada ya marudio Mtumbuka akafanikiwa kuchukua kijiti hicho cha kuiwakilisha CCM katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Kijiji na Kitongoji utakaofanyika nchini kote Novemba 27 mwaka huu.


Pia katika nafasi ya uenyekiti wa Kijiji cha Kazole Kata ya Vikindu kupitia CCM,  itawakilishwa na Mohamed Kitage.


Mtambuka, akizungumza na mwandishi wetu, amesema kuwa  anawashukuru wajumbe kwa kumuamini na kumpa nafasi ya kukiwakilisha kitongoji hicho kupitia CCM katika uchaguzi ujao.


"Uchaguzi wa kura za maoni ndani ya chama, umekwisha nawaomba wanachama wote tuvunje makundi na tuwe kitu kimoja ili tufanikishe kupata ushindi katika uchaguzi ujao," amesema.




No comments:

Post a Comment