NAIBU WAZIRI KAPINGA ASHIRIKI JUKWAA LA MAWAZIRI NCHINI AFRKA KUSINI - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Tuesday, October 8, 2024

NAIBU WAZIRI KAPINGA ASHIRIKI JUKWAA LA MAWAZIRI NCHINI AFRKA KUSINI


NA MWANDISHI WETU

NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameshiriki Jukwa la Mawaziri (Ministerial Symposium)  nchini Afrika Kusini ikiwa ni sehemu  Kongamano la Wiki ya Mafuta Afrika (Afrika Oil Week) linalofanyika Jijini Cape Town.


Jukwaa hilo pia limehudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Dkt. James Mataragio, Kamishina wa Petroli na Gesi Ndg. Goodluck Shirima na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli ( PURA), Mha. Charles Sangweni.


Maudhui ya Kongamano hilo ni pamoja na kutangaza fursa za uwekezaji katika miradi ya Mafuta, Gesi Asilia na Nishati Mbadala katika Bara la Afrika.


Kongamano hilo litamalizika kesho, Oktoba 10, 2024 nchini humo.









No comments:

Post a Comment