NA MWANDISHI WETU
MTUMISHI wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) Wilaya ya Kinondoni, Hamphrey Einhrad Haule amefikishwa katika Mahakama ya Kinondoni na kufunguliwa shauri la Uhujumu Uchumi namba 'ECC. 28546/2024'
Katika Shauri hili inaelezwa kuwa mshtakiwa Humphrey akiwa Ofisa Usajili chini ya Kitengo cha Utawala na Fedha pamoja na majukumu mengine alipangiwa majukumu ya kushughulikia safari za kikazi kwa watumishi wa NIDA.
Akitekeleza jukumu hilo, alifanya ubadhirifu wa fedha za safari za viongozi wa NIDA na kuzitumia kwa manufaa yake binafsi na hivyo anashtakiwa kwa makosa ya kufanya ubadhirifu wa dolla za kimarekani USD 8,779 kinyume na K/f cha 28(1)cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura ya 329 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2022 na kosa la wizi kwa mtumishi wa umma k/f 270 cha Sheria ya Kanuni za Adhabu Sura ya 16 Marejeo ya 2022 .
Aidha, Shauri tajwa limesomwa mahakamani hapo na mshtakiwa amekana makosa yote na kushindwa kutimiza masharti ya dhamana hivyo kupelekwa Rumande.
Kesi hii imesomwa na waendesha mashitaka kutoka TAKUKURU Kinondoni Wakili *Aidan Samali na Thuwaiba Hussein* mbele ya Mhe. Ramadhan Lugemalira Hakimu Mfawidhi Wilaya ya Kinondoni
Kesi hiyo itakuja tena Mahakamani tarehe 22/10/2024 kwa ajili ya kusomwa hoja za awali.
%20(1).jpeg)




No comments:
Post a Comment