NA MAGENDELA HAMISI
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajia kuwa mgeni rasmi katika Ibada ya Misa Maalim ya kusheherekea Jubilee ya miaka 50 ya Africa Inland Church Tanzania (AICT), Oktoba 27, 2024.
Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es Salaam na Baba Askofu, Phillip Magwano wa Kanisa la AICT - Dayosisi ya Pwani na akafafanua kwamba misa hiyo itafanyika katika hilo, Magomeni Mzimuni jijini Dar es Salaam.
"Tunayofuraha kuwataarifu waumini wote wa AICT na watanzania kwa ujumla kwamba mgeni rasmi anatarajiwa kuwa, Rais Dkt Samia na amekubali kujumuika nasi kwenye misa hiyo itakayoenda sambamba na harambee ya kukamilisha ujenzi letu unaondelea kwa sasa," amesema.
Ameongeza kuwa kuelekea siku hiyo, kutakuwa na shughul mbalimbali ikiwemo tamasha la Uimbaji, maombi na shughuli za kijamii na matendo ya huduma na upendo kwa jamii ya watanzania wanaoishi katika mazingira magumu ambapo watashikwa mkono kwa kupatiwa mitungi ya gesi ili kuunga mkono juhudi za Rais Samia katika agenda ya Nishati Safi.
"Pia kwa unyenyekevu mkubwa katika jina la Yesu, nawaalika watanzania wote mje kushiriki pamoja katika ibada hiyo maalum, tulitukuze na kuliinua na kulisifu na kuliabudu jina la Mungu wetu, aliyehai kwa kazi ya Neno lake iliyofanyika kwa miaka 50," amesema.
Ameongeza kuwa katika misa hiyo itakayofanyika ndani ya Kanisa la AICT - Magomeni itaambatana na kumtukuza, kumsifu na kumwabudu Mungu kwa mahubiri, nyimbo, maonesho maalumu na ujumbe maalumu kwa mgeni rasmi.
Pia amesema itakuwa ni fursa adhimu na adhimu ya kuungana na marafiki wa zamani, kufurahi pamoja katika imani na kufikiria mustakabali wa kanisa Hilo.





No comments:
Post a Comment