RC SENDIGA: UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA UTAKUWA WA HAKI VIJANA JITOKEZENI - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Monday, October 21, 2024

RC SENDIGA: UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA UTAKUWA WA HAKI VIJANA JITOKEZENI

 


NA MWANDISHI WETU

WANANCHI wa Mkoa wa Manyara hususan vijana, wametakiwa kujiandikisha katika Daftari la Makazi kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa 2024, ili wapate nafasi ya kuwaondoa viongozi wasiosimamia maslahi ya wananchi.


Wito huo ulitolewa hivi karibuni na Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga, alipowatembelea vijana wanaocheza 'Pool Table' mjini Dongobesh wilayani Mbulu.


"Lazima mkajiandikishe na mpige kura ya kuwatoa msiowapenda, msipoenda kujiandikisha tutaenda kuwatoaje? Tutawatoa kwa kukaa humu ndani tunacheza pool? Hawawezi kutoka," alisema Sendiga na kuongeza:


"Kwa hiyo tusipowatoa tutaanza kulalamika huyu Mzee anatudhurumu sasa wakati wa kumshughulikia ndio huu, bila kujiandikisha na kupiga kura hatuwezi hamuwezi kuchagua kiongozi mnayemtaka."


Mkazi wa Dongobesh,Tumaini Wilson Doita, alisema vijana wengi walikuwa hawana mwamko wa kwenda kujiandikisha wakidhani uchaguzi hautakuwa huru na wa haki lakini baada ya kuhakikisha utakuwa wa haki wamehamasika kushiriki zoezi hilo.

No comments:

Post a Comment