TBA KUANZA KUWAONDOA WADAIWA SUGU OKTOBA 7 MWAKA HUU - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Wednesday, October 2, 2024

TBA KUANZA KUWAONDOA WADAIWA SUGU OKTOBA 7 MWAKA HUU


NA MAGENDELA HAMISI


WAKALA wa Majengo Tanzania (TBA) wanatarajia kuendesha operesheni ya kuwaondoa wadaiwa sugu Oktoba 7 mwaka huu na wataanza katika mikoa minne ambayo ni Arusha, Mwanza, Dodoma na Mara.

Pia imeelezwa kwamba licha ya kuwaondoa wadaiwa hao katika nyumba hizo, hatua nyingine itakayofuata kwa atakayeshindwa kulipa deni atafikishwa mahakani.


Mkurugenzi Mkuu wa TBA, Arch Daud Kondoro amebainisha hayo leo, jijini Dar es Salaam na akafafanua kwamba hatua hiyo ya kuwaondoa wadaiwa sugu imekuja baada ya kuwapa notisi ya siku saba.

Ameongeza kuwa wadaiwa sugu wanaotarajiwa kuondoshwa ni 648 ambao tayari wamepewa notisi ya wiki mbili ili kufanikisha mchakato wa kulipa deni ambayo ni Shilingi bil 14.8.

Ameongeza kuwa katika mikoa hiyo minne deni ambao wateja wanadaiwa ni bil 1.7 na tunawataka kuhakikisha wanalipa kwa wakati mara baada ya kupokea ujumbe mfupi wa kumbukumbu ya malipo ambayo utumwa kwao kila mwezi.9

"Kwakweli changamoto ya madeni kwa wapangaji imekuwa ni sugu na hatua kadhaa zimekuwa zikichukukuwa kudhibiti hilo, moja ni kuwaondoa katika nyumba na kabla ya kuwafikisha mahakamani huwa tunazungumza nao namna watakavyoweza kulipa," anasema.


Ameongeza kuwa jukuku la kuwaondoa wadaiwa hao sugu wamekabidhiwa dalali wa Mahakama, Twins Action Mart na wapo tayari kutekeleza jambo hilo.


Ameongeza ili kukabiliana na mchakato wa kukusanya madeni hususan kwa watumishi wa Serikali wamewekewa mfumo wa kieletroniki wa Usimamizi wa Miliki za Serikali (GRMS) utakaosaidia kuboresha ukusanyaji wa kodi.

Mfumo huo utawawezesha watumishi wa umma, kulipa kodi moja kwa moja kutoka kwenye mishahara yao.


Arch Kondoro amefafanua kwamba ili kwa sasa wanaendelea na mchakato wa kufunga vitasa janja na smart meter katika nyumba hizo kwa lengo kuimalisha ukusanyaji madeni kwa wadaiwa sugu

Pia wapangaji na wadaiwa sugu, wamesisitizwa kufuatilia taarifa zao kupitia mtandao rasmi wa kijamii wa TBA na si vinginevyo. 


No comments:

Post a Comment