WALIMU WA KIKE WAITWA KUFUNDISHA CHUO CHA UFUNDI FURAHIKA - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Tuesday, October 15, 2024

WALIMU WA KIKE WAITWA KUFUNDISHA CHUO CHA UFUNDI FURAHIKA


NA MWANDISHI WETU

UONGOZI wa Chuo cha Ufundi cha Furahika ambacho kinapatikana Buguruni Malapa jijini Dar es Salaam kinahitaji walimu wa kike wa kujitolea kufundisha masomo ya Compyuta, Bandari, Hoteli, Ususi na Sekretari na watakaofanya vizuri watapewa mkataba wa ajira chuoni hapo.


Kaimu Mkuu wa Chuo, hicho Dkt David Msuya amebainisha hayo leo jijini Dar es Salaam alipozungumza na Mwandishi Wetu na kufafanua kwamba walimu wa masomo hayo wanaohitajika haraka kulingana na mahitaji ya chuo hicho.


“Hao walimu wanaohitajika wa kike kwa ajili ya kufundisha masomo hayo kwa kujitolea na watakaofanya vizuri tutawapa mkataba na kigezo cha kwanza wajitolee kufundisha vijana wetu na tutakuwa tukifuatilia uwezo wao wa kufundisha  na tutakaoridhika  nao tutawapa mkataba wa ajira ” amesema.

No comments:

Post a Comment