WIZARA YA NISHATI NA UNDP ZAWANOA WATAALAM MATUMIZI BORA YA NISHATI - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Wednesday, October 2, 2024

WIZARA YA NISHATI NA UNDP ZAWANOA WATAALAM MATUMIZI BORA YA NISHATI


Kaimu Kamishna Msaidizi wa Nishati Jadidifu kutoka Wizara ya Nishati, Mhandisi Imani Mruma,  akizungumza na Wadau wakati akifunfua Mafunzo ya Mpango Kazi wa Utekelezaji wa Matumizi bora ya Nishati Tanzania yanayofanyika tarehe 1 hadi 3 Oktoba, Mkoani Morogoro.


 NA MWANDISHI WETU, MOROGORO


WIZARA ya Nishati kwa kushirikiana na  Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) wameandaa warsha itakayowawezesha Wataalam kutoka Taasisi mbalimbali za Serikali kupitia  nyaraka zitakazowezesha kuandaa vigezo vya kitaalam vitakavyoongoza kazi ya usimamizi na ukaguzi wa matumizi bora ya nishati nchini.


Warsha hiyo imehusisha wadau mbalimbali ikiwemo Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO), Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).


Pia Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi( VETA), Taasisi ya Elimu ya Juu Tanzania(TCU) na Baraza la Taifa la Elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi (NACTVET).


Akizungumza katika warsha hiyo mkoani Morogoro, Oktoba 2, 2024, Kaimu Kamishna Msaidizi wa Nishati Jadidifu kutoka Wizara ya Nishati, Mhandisi Imani Mruma, amesema warsha hiyo imezilenga zaidi Taasisi zinazosimamia matumizi bora na sahihi ya nishati nchini.


Amesema baada ya warsha hiyo, wadau hao kwa pamoja watatoa andiko la namna bora ya kusimamia ubora wa bidhaa za nishati nchini pamoja na ukaguzi wake.


"Azma ya Serikali ni kuhakikisha kuwa kila mtanzania anapata nishati kwa uhakika, kwa gharama nafuu na uendelevu hivyo mafunzo kwa wadau mbalimbali ni muhimu ili kuchagiza utekelezaji wa haraka wa ajenda ya matumizi bora ya nishati." Amesisitiza Mha.Mruma


Kwa upande wake, Meneja wa Utekelezaji wa Matumizi Bora ya Nishati kutoka UNDP, Aaron Cunningham amesema uandaaji wa vigezo vya kitaalam na ujuzi katika kusimamia na kukagua matumizi ya nishati vinalenga kuandaa Wataalam ambao watasaidia nchi kufanya ukaguzi na usimamizi wa matumizi bora ya nishati. 


"Warsha hizi ni endelevu na kwa kutumia warsha kama hii ya leo,  tumeweza kupata miongozo mitatu kwa ajili ya kuandaa wataalamu hao. Miongozo hii itatumika nchi nzima na kutekelezwa na wadau mbalimbali wa nishati na elimu." Amesema Cunningham.


Ameongeza kuwa, UNDP kama mdau wa Maendeleo, itaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania ili kuweka mazingira rafiki na rahisi katika masuala ya matumizi bora ya nishati pamoja na upatikanaji wake.

Meneja wa Mradi wa Utekelezaji wa Matumizi bora ya Nishati Tanzania, kutoka Shirika la Maendeleo( UNDP)Aaron Cunningham akizungumza na Wadau wakati wa mafunzo ya Mpango Kazi wa Utekelezaji wa Matumizi bora ya Nishati Tanzania yanayofanyika tarehe 1hadi 3 Oktoba, Mkoani Morogoro.

Mtaalamu wa Matumizi Bora ya Nishati, Sayuni Mbwilo kutoka Shirika la Maendeleo(UNDP) akizungumza na Wadau wakati Mpango wa Utekelezaji wa Matumizi bora ya Nishati, Tanzania kwa Wadau wa Nishati,  yanayofanyika tarehe 1hadi 3 Oktoba, Mkoani Morogoro.


Kaimu Kamishna Msaidizi wa Nishati Jadidifu, kutoka Wizara ya Nishati, Mhandisi Imani Mruma(katikati)akiwa katika picha ya Pamoja na wadau mbalimbali wakati wa

Mafunzo ya  Mpango wa Utekelezaji wa Matumizi bora ya Nishati, Tanzania kwa Wadau wa Nishati,  yanayofanyika tarehe 1hadi 3 Oktoba, Mkoani Morogoro.

No comments:

Post a Comment