WAZIRI CHANA AINADI CCM MAKAMBAKO, AMTAJA RAIS DKT SAMIA - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Monday, November 25, 2024

WAZIRI CHANA AINADI CCM MAKAMBAKO, AMTAJA RAIS DKT SAMIA


NA MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Njombe, Balozi , Dkt. Pindi Chana (Mb) amekinadi Chama cha Mapinduzi huku akiwaomba wananchi kuchagua wagombea wa CCM katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 27,2024.


Ameyasema hayo katika Mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Lyamkena, Halmashauri ya Mji wa Makambako Mkoani Njombe leo Novemba 25, 2024.


Amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa fedha za miradi mbalimbali ya maendeleo Mkoani humo katika Wilaya zote za Makambako, Ludewa, Njombe na Wanging'ombe  za ujenzi wa barabara , shule , vituo vya afya n.k.


Akizungumzia Sekta ya Maliasili na Utalii, Chana amesema Rais Samia amekuwa kinara katika kutangaza vivutio vya Tanzania hasa kupitia filamu ya Tanzania The Royal Tour.




No comments:

Post a Comment