NA MWANDISHI WETU
KATIBU Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi leo Disemba 9, 2024 amesherehekea miaka 63 ya Uhuru kwa kutembelea Pori la Akiba la Pande lililopo nje kidogo ya jijini la Dar es salaam na kuzungumza na Menejimenti pamoja na watumishi akihimiza kuvutia watalii zaidi wa ndanilakini na nje pia.
Akizungumza na Menejimenti ya Pori hilo, Dkt. Abbasi ameelekeza kuboreshwa kwa miundombinu ya pori hilo pamoja na kuongeza wanyamapori zaidi ili wananchi wa Dar es salaam na mikoa ya jirani waweze kutalii katika eneo hilo.
Amesisitiza pia watumishi kuzingatia maadili katika utendaji wa kazi zao na kufanya kazi kwa bidii na weredi ili kuendeleza pori hilo ili liweze kuongeza idadi ya watalii wa ndani na mapato.
Pori la Akiba la Pande linatupatia fursa ya kufanya utalii wa Bustani ya Wanyamapori Hai kama Simba, Duma,Chui, Nyumbu, Pundamilia, Swala,Chatu na Ndege wa aina mbalimbali lakini na maeneo ya kambi maalum, mbio za baiskeli,sherehe mbalimbali na matembezi ya msituni ili kujenga afya.
Baada ya maelekezo ya Katibu Mkuu ,neno la shukrani likatolewa na Kamishna Msaidizi Mwandamizi Sylivester Mushy (Kamanda wa Uhifadhi -Kanda Maalum ya Dsm).
kwa kumshukuru Dkt.Abbasi kwa kutembelea Pori la Akiba Pande.
Mushy Kwa niaba ya watumishi amehaidi kutekeleza maelekezo yake aliyetoa kwa watumishi.
No comments:
Post a Comment