EWURA YATOA RAI WANANCHI KUVUNA MAJI YA MVUA KUONDOA MALALAMIKO KWA SERIKALI - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Friday, December 13, 2024

EWURA YATOA RAI WANANCHI KUVUNA MAJI YA MVUA KUONDOA MALALAMIKO KWA SERIKALI


NA MWANDISHI WETU

WANANCHI wametakiwa kuvuna na kuhifadhi maji mvua kwa kutumia matenki au visima vitakavyowawezesha kuwa na huduma hiyo kwa kipindi chote cha mwaka jambo litakaloondoa malalamiko kwa Serikali kwa maeneo ambayo huduma hiyo ina changamoto au haijafika.

Pia itasaidia kuwaondolea wananchi malalamiko ama adha ya kubambikiziwa bili kubwa kutoka kwa baadhi ya Mamlaka za Maji ambazo zimekuwa zikilalamikiwa kutoa bili za maji tofauti na matumizi halisi ya mlaji.

 Meneja Mawasiliano na Uhusiano, Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji EWURA, Titus Kaguo, ametoa wito huo leo jijini Dar es Salaam, Desemba 13, 2024 wakati wa Semina ya Mafunzo ya Udhibiti wa Huduma za  Nishati na Maji ambayo wameitoa kwa wananchama wa Chama cha Wafanyakazi wa Vyombo vya Habari Tanzania (JOWUTA).

“Kumekuwa na malalamiko kwa Serikali katika maeneo ambayo huduma ya usambazaji maji ina changamoto, pia hata kwa wateja ambao waoletewa bili za maji wapo ambao wanalalamika kuzidishiwa tofauti na matumizi yao.

“Hali hiyo itasaidia kuondoa malalamiko hayo kwa Serikali hususan katika maeneo ambayo yanachangamoto ya upatikanaji wa huduma hiyo na Mamlaka za Maji kuhusu madai ya baadhi ya wateja kuzidishiwa bili tofauti na matumizi yao”, amesema.  

Kagua ambaye katika semina, hiyo alimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Dkt James Andilile, ameongeza kuwa licha ya kuondoa malalamiko hayo, pia kuhifadhi maji ya mvua kwa matumizi itawasadia kutumia fedha iliyokuwa itumike kwa ajili ya kulipia maji kutumika katika matumizi mingine.






No comments:

Post a Comment