OFISI YA WAZIRI MKUU YATOA TAARIFA UWEPO WA KIMBUNGA 'CHIDO' KATIKA BAHARI YA HINDI KASKAZINI MWA MADAGASCAR - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Thursday, December 12, 2024

OFISI YA WAZIRI MKUU YATOA TAARIFA UWEPO WA KIMBUNGA 'CHIDO' KATIKA BAHARI YA HINDI KASKAZINI MWA MADAGASCAR


 NA MWANDISHI WETU

OFISI ya Waziri Mkuu inatoa taarifa kwa umma kufuatia tahadhari iliyotolewa na Mamlaka
ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kuhusu uwepo wa kimbunga “CHIDO” katika Bahari ya Hindi kaskazini mwa kisiwa cha Madagascar.

 Kimbunga hicho kinatarajiwa kuelekea
maeneo ya kaskazini mwa Msumbiji katika kipindi cha siku nne zijazo (tarehe 13 hadi 16
ya mwezi Disemba, 2024).

Aidha, kwa sasa, kimbunga hicho hakiashirii uwezekano wa kusababisha athari za moja kwa moja hapa nchini. 

Hata hivyo, kutokana na ukaribu wa maeneo ambayo kimbunga“CHIDO” kinatarajiwa kupita (kaskazini mwa Msumbiji) na maeneo ya kusini mwa nchi yetu, upo uwezekano mdogo wa matukio ya vipindi vifupi vya mvua kubwa itakayoambatana na upepo mkali na mawimbi makubwa ya bahari kwa maeneo ya Mtwara na maeneo jirani hususan kati ya tarehe 14 na 16 ya Disemba 2024.

USHAURI: 

Wananchi wanaoishi kando kando ya bahari, watumiaji wa bahari na wananchi
wengine waliopo katika mikoa ya kusini wanashauriwa kuchukua tahadhari na kuendelea
kufuatilia na kuzingatia taarifa za utabiri kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania.

 Vilevile, Mamlaka za Serikali za Mitaa zikiongozwa na Kamati za Usimamizi wa Maafa katika ngazi za mikoa, wilaya, kata na kijiji/mtaa zinatakiwa kuchukua hatua za tahadhari na kusimamia utekelezaji wake kwa wananchi waliopo katika maeneo yao.

Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inaendelea kufuatilia kwa ukaribu mwenendo wa kimbunga hicho.

No comments:

Post a Comment