TANZANIA KUZINDUA TUZO ZA UTALII NA UHIFADHI DISEMBA 20 , 2024 MWAKA HUU - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Sunday, December 8, 2024

TANZANIA KUZINDUA TUZO ZA UTALII NA UHIFADHI DISEMBA 20 , 2024 MWAKA HUU


NA MWANDISHI WETU

WIZARA ya Maliasili na Utalii, imesema kuwa itaendelea kuumga mkono juhudi za serikali chini ya raisi wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia suluhu Hassan katika kukuza sekta ya utalii ndani na nje ya nchi


Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt.Hassan Abbas wakati akitangaza kufanyika kwa uzinduzi wa Tuzo ya Utalii na Uhifadhi itakayofanyika Disemba 20 ,2024 mwaka huu jijini Arusha.

Amesema kwamba hiyo ni mara ya kwanza kwa Tanzania kutoa tuzo kwa wadau mbalimbali wa sekta ya utalii ambao wanakumbukwa kwa kutoa mchango ulioiwezesha sekta hiyo kuwa na mafanikio.


Katika hatua nyingine Dkt. Abbas ameweza kuzungumzia tuzo ambazo nchi imezipata dunianí na Afrika kiujumla ambazo zimetokana na kuwa na vivutio bora na kuchangia pato la Taifa Katika nyanja mbalimbali za kiutalii na akatatolea mfano mbuga za wanyama kama Serengeti , Ruaha, Ngorongoro pamoja na kuwepo na makumbusho ya kale ni miongoni mwa vitu vinavyosababisha Taifa kuwa na vivutio katika suala zima la kuingiza watalii nchini

No comments:

Post a Comment