MGANGA Mkuu wa Serikali Prof. Tumaini Nagu akiwa nchini Uingereza kwenye ziara ya Waziri wa Afya, Jenista Mhagama ametembelea Hospitali ya Imperial Collage Health Care (NHS) iliyopo katika mji wa London.
Pamoja na mambo mengine Prof. Nagu amezungumza na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara katika Hospitali NHS Dkt. Alistair Russell juu ya kubadilisha uzoefu kwa wataalamu wao na Watanzania ili kuweza kufanya kazi pamoja ya kuwahudumia wananchi wao katika Sekta ya Afya.
Miongoni mwa mambo mengine waliyojadiliana ni pamoja na kufanya tafiti za masuala ya afya ikiwemo ya magonnwa yasiyoambukiza katika kuelekea utekelezaji wa Bima ya Afya kwa Wote ili kila Mtanzania apate huduma za afya bila kikwazo cha fedha.
No comments:
Post a Comment