JOWUTA YATOA RAI KWA VYAMA VYA SIASA KUWALINDA WAANDISHI - MAGENDELA BLOG

Recent-Post

ads header

Thursday, April 24, 2025

JOWUTA YATOA RAI KWA VYAMA VYA SIASA KUWALINDA WAANDISHI


 NA MWANDISHI WETU, MOROGORO


MWENYEKITI wa Chama cha Wafanyakazi wa Vyombo vya Habari Tanzania (JOWUTA), Mussa Juma ametoa wito kwa viongozi wa vyama vya siasa nchini kuhakikisha wanawalinda Waandishi katika uchaguzi mkuu ujao.


Uchaguzi Mkuu nchini unatarajiwa kufanyika nchini Oktoba mwaka huu, Mwenyekiti huyo wa Jowuta, Juma ametoa wito huo leo Aprili 24 mwaka huu mkoani Morogoro wakati akifunga mafunzo ya kuwajengea uwezo wanachama wake ili waweze kuandika habari kwa kufuata misingi ya tasnia hiyo.


"Kumekuwa na tabia kadhaa zikitokea hususani katika kipindi cha chaguzi ambapo baadhi ya waandishi wamekuwa wakipitia changamoto nyingi ikiwemo kufukuzwa kwenye misafara ya vyama vya siasa kutokana na kuandika taarifa kinyume mahitaji ya vyama hivyo.


"Kulingana na changamoto hizo ambazo zimekuwa zikiwaondolea uhuru waandishi, tunaviomba vyama vya siasa wawalinde waandishi ili wawe huru kutumia kalamu yao vizuri bila bugudha, "amesema.


Pia hakusita kusema kuwa nao waandishi wanatakiwa kuandika habari zinazohusisha uchaguzi kwa kufuata misingi ili kuepuka changamoto zinazoweza kujitokeza na kuziweka nchi salama.


Mafunzo hayo ambayo yanaratibiwa na JOWUTA ni ya awamu ya kwanza yamefanyika kwa wanachama wao wa kanda ya Dar es Salaam na Pwani na itaafuta Kanda ya Nyanda za Juu Kusini na Kanda ya Kaskazini.


Jowuta inatoa mafunzo hayo kwa  kushirikiana na Shirikisho la Kimataifa la Waandishi Duniani(IFJ) ambao ndio wadhamini wakuu na wengine ni Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binaadamu(THRDC) ni Shirikisho la Waandishi Afrika(FAJ) na MAIPAC.


Ikumbukwe kuwa Uchaguzi Mkuu nchini Tanzania unafanyika kila baada ya Miaka mitano  na unahusisha kumchagua Rais, Wabunge na Madiwani.



No comments:

Post a Comment