DKT. NA MWANDISHI WETU
KADA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Angelo Nyonyi, amechukua fomu ya kuwania Jimbo la Kibamba jijini Dar es Salaam
Akizungumza wakati akitoka kuchukua fomu ya kuwania nafasi hiyo ya kutumikia wananchi katika jimbo hilo, Dkt Nyonyi, amesema kwamba baada ya kujithimini, anaamini kwamba anaweza kuongoza nafasi hiyo.
"Kikubwa leo, nimekuja kuchukua fomu ikiwa ni hatua ya awali ya mchakato huu wa kutia nia kugombea Jimbo hili la Kibamba, hivyo tusubiri jina langu likirudi ndipo nitakuwa na fursa ya kusema hatua nitakazochukua ikiwa nitachaguliwa kuwa mbunge," amesema
No comments:
Post a Comment