NA MWANDISHI WETU
DKT. David Chintelele, ametumia haki yake ya msingi kama kijana kujitokeza kutia nia ya kugombea ubunge Jimbo la Kibamba, jijini Dar es Salaam.
Kada huyo wa CCM, amefafanua kwamba anashukuru fursa iliyopo kwenye chama chake ambayo inatoa nafasi kwa vijana na makundi mbalimbali kuomba nafasi ya kuchaguliwa na kuchagua viongozi
"Mimi kama kijana, nimeamua kutumia fursa iliyotolewa na chama changu kuingia kwenye uchaguzi na ikiwa nitapata nafasi niweze kuwatumikia wananchi wa jimbo hili la Kibamba
"Hivyo leo, nimekuja kuchukua fomu kwa ajili ya kuomba nafasi katika chama ili kugombea Jimbo hili la Kibamba, hivyo nitasema mikakati na sera zangu na nini nitafanya baada jina langu kurudi na muda wa kampeni ukifika," amesema.





No comments:
Post a Comment