NA MWANDISHI WETU
MWALIMU Baraka Kagoma ambaye ni Mwenyekiti Jumuia ya Wazazi Makondeko Kata ya Kwembe jijini Dar es Salaam, amejitosa kuchukua fomu ya kuwania ubunge Jimbo la Kibamba.
Kada huyo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), licha ya kuwa na nafasi hiyo, pia aliwahi kuwa mgombea udiwani mwaka 2020 katika ya Kwembe.
Aidha wakati akiwa anasoma Chuo Cha St. Joseph alipata nafasi ya kuwa Waziri Mkuu chuoni hapo kuanzia mwaka 2018 hadi 2021 na Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM.
Kutokana na muktadha huo, Mwl Kagoma, amejipima na kuamini kuwa na uwezo wa kuongoza kuchukua fomu ikiwa atafanikiwa kupata ridhaa ya wajumbe kuwa mgombea ubunge wa Jimbo hilo.
No comments:
Post a Comment