NA MWANDISHI WETU
CHAMA Cha Ukombozi wa Umma (CHAUMA) kimeendelea kuvunja
ngome ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) baada ya leo Kada
kindakindaki wa CDM kutoka mkoani Njombe, Sigrada Mligo kujiunga rasmi na chama
hicho.
Sigrada kabla ya kujiunga CHAUMA, alikuwa ni Katibu Mwenezi
wa Baraza la Wanawake Taifa (BAWACHA) ingawa pia alishawahi kushika nyadhifa
mbalimbali akiwa CHADEMA ikiwemo Udiwani Viti Maalumu.
Tofauti hayo kada huyo ambaye kwa sasa ni mwanachama rasmi
wa CHAUMA baada ya kukakibidhiwa kadi na Katibu Mkuu wa chama hicho, Salum
Mwalimu, amesema ameamua kuondoka CHADEMA baada ya kudaiwa kutumika na anataka
kukiua chama hicho alichokitumikia kwa jasho na damu tangu mwaka 2011 akiwa
chuoni.
.
“Haikuwa kazi rahisi kufanya maamuzi haya, nimetafakari sana
baada ya kupigwa na kuumizwa vibaya nje ya mkutano huku baadhi ya viongozi
wakiaminika ndio waliopanga njama hizo na hatimaye kumtorosha mtuhumiwa.
“Pia hawakuhusika katika matibabu yangu hata kidogo, huku
Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakachukua nafasi hiyo kwa kunikodishia gari ya
wagonjwa na kunipatia Shilingi 1,500, 000 za matitabu ambazo baadhi nilizitumia
kulipa deni la hoteli ambalo CHADEMA walikuwa wakidaiwa na baadhi nililipia
gharama za matibabu.
“CHADEMA nimekifanyia mengi ikiwemo ujenzi chama kwa fedha
zangu, wageni wote wa chama waliokuwa wakifika Njombe,Mimi nilikuwa
nawagharamia kila kitu lakini leo thamani yangu haionekani, natuhumiwa
kukihujumu chama na kutaka kukiua sasa kabla hakijafa naamua kujiondoa ili
maneno yao yasitimie nikiwepo, ukweli nimepoteza uhalali wa kuwa chadema kutokana
na kauli hizo.
“Pia nimefadhili operesheni mbalimbali cha kujenga chama kwa
fedha zangu binafsi na nimetumia zaidi ya
Sh. milioni 15 kuhakikisha majimbo
matatu ya Mkoa wa Njombe yanashiriki mchakato wa uchaguzi wa ndani ya chama na
hakuna anayeweza kubisha kwani kumbukumbu zipo,” amasema.
Hatua hiyo ya kujiengua CHADEMA kwa kada huyo inakuja miezi
kadhaa baada ya kudaiwa kujeruhiwa na
mmoja wa walinzi wa Chadema wakati wa kikao cha ndani kilichoongozwa na Makamu
Mwenyekiti, John Heche, Machi 25, 2025, mkoani Njombe.
Katika mkutano alioufanya leo Julai 27, 2027 na Waandishi wa
Habari, jijini Dar es Salaam Sigrada alifafanua kuwa wakati wa Uchaguzi Mkuu uliopita
wa Chadema, alikiri kuwa kambi iliyomuangusha aliyekuywa Mwenyekiti, Freeman
Mbowe kutokana na kuwepo kwa ahadi kedekede ambazo hadi sasa zimekuwa hewa na
chama kuendeshwa kiharakati badala ya kimkakati.
Kulingana na hayo kwa sasa anamuomba aliyekuwa Mwenyekiti wa
CHADEMA, Mbowe naye achukue maamuzi magumu kwa maana yaliyotarajiwa wakati wa
uchaguzi si haya yanayoendelea sasa.
No comments:
Post a Comment