KATIBU MKUU TAASISI SAMIA FOR US TAIFA ACHUKUA FOMU JIMBO LA KIBAMBA - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Tuesday, July 1, 2025

KATIBU MKUU TAASISI SAMIA FOR US TAIFA ACHUKUA FOMU JIMBO LA KIBAMBA


 NA MWANDISHI WETU


KATIBU wa Taasisi ya Samia For Us Taifa inayoratibu na kuendesha kampeni ya Mama Samia Asemewe, Dwight Danda amejitokeza kuchukua fomu ya kuwania Jimbo la Kibamba jijini Dar es Salaam.


Kada huyo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), amekuwa mtia nia mdogo zaidi kati ya waliojitokeza kuchukua fomu kwa ajili ya kuomba nafasi ya kuwania ubunge wa jimbo hilo.


"Leo Julai Mosi, 2025 nimeamua kutumia fursa kama kijana kutia ni ya kugombea ubunge katika Jimbo la Kibamba naamini ikiwa jina langu litapita nitaweka wazi mikakati yangu na kuanza kampeni muda utakapofika," amesema.

Hadi sasa Danda ndio mtia ni pekee mwenye umri zaidi ya waliojitokeza kuchukua fomu kwa ajili ya kuomba ridhaa ya kuchaguliwa na wajumbe kugombea Jimbo hilo.

No comments:

Post a Comment