TUNAHITAJI JITIHADA ZA PAMOJA KUPAMBANA NA UDUMAVU – DKT. YONAZI - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Tuesday, July 29, 2025

TUNAHITAJI JITIHADA ZA PAMOJA KUPAMBANA NA UDUMAVU – DKT. YONAZI


NA MWANDISHI WETU

KATIBU Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dkt. Jim Yonazi, ametoa wito kwa Serikali na wadau kushirikiana kwa karibu katika mapambano dhidi ya tatizo la udumavu nchini.


Akizungumza katika kikao cha maandalizi ya Mkutano Mkuu wa 11 wa Wadau wa Lishe nchini, kinachotarajiwa kufanyika Septemba 4–5, 2025 jijini Dar es Salaam, Dkt. Yonazi amesema juhudi za pamoja, tafiti, elimu na majukwaa ya kitaifa ni muhimu katika kutokomeza udumavu.


Mkutano huo wa kitaifa unatarajiwa kufunguliwa rasmi na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Kassim Majaliwa.




No comments:

Post a Comment