WANAFUNZI MISRI WAZINDUA MPANGO WA 'DIPLOMASIA YA AFYA' - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Wednesday, July 9, 2025

WANAFUNZI MISRI WAZINDUA MPANGO WA 'DIPLOMASIA YA AFYA'


NA MWANDISHI WETU 

WANAFUNZI nchini Misri wamezindua toleo la kwanza la Mpango wa 'Diplomasia ya Afya' kwa wanafunzi wa tiba ambao ni wa kwanza wa aina yake nchini Misri na Afrika.


Mpango wa kwanza nchini humo udhamini wa Muungano wa Kimataifa wa Wanafunzi wa Tiba Misri na tawi lake katika Chuo Kikuu cha MTI, kwa usaidizi wa Jumuiya ya Kisayansi ya Wanafunzi wa Tiba.


Pia mpango huo umepata ufadhili wa vyombo vya habari kutoka kwa Mpango wa Afromedia wa Uandishi wa Habari na Mawasiliano kwa ajili ya kuelimisha na kutangaza nafasi na uwezo wa daktari katika jamii yake.


Wafadhili wengine ni Chuo cha Tiba ya Binadamu cha Chuo Kikuu cha Kisasa cha Teknolojia na Habari ambacho kiliandaa shughuli za mpango huo, kama sehemu ya juhudi za dhahiri za kuwawezesha madaktari chipukizi na wanafunzi wa tiba kutoka Misri pamoja na wanafunzi kutoka Sudan.


Mpango huo umelenga kuwapatia mazingira ya kujifunza yaliyo jumuishi na ya haki kwa wakimbizi wa vita vya Sudan, yanayochanganya kati ya elimu ya kitaaluma na uzoefu wa vitendo.


Aidha, mpango huu umesanifiwa kwa lengo la kuwawezesha wanafunzi wa tiba nchini Misri, huku ukitoa fursa sawa na za haki kwa wanafunzi na madaktari wa Kiafrika wasio Wamisri wanaoishi nchini Misri, ili kupata uelewa wa kina kuhusu nyanja mbalimbali za afya na muktadha wake wa Kiafrika na kimataifa, mahusiano ya kimataifa na sera za afya.


Pia, kuwapa ujuzi wa kufanya utafiti utakaowawezesha kushiriki kikamilifu katika mzunguko wa maamuzi ya kisera ya afya katika ngazi ya kitaifa na kimataifa.


Mpango huo ulihusisha ushiriki wa kundi la wasemaji na wataalamu mashuhuri kutoka sekta mbalimbali, wakiongozwa na Mostafa Magdy, Msaidizi wa Waziri wa Vijana na Michezo,  Dk Samah Kamel, Mkuu wa Kikundi cha Vijana na Watoto wa Umoja wa Mataifa, na Dk Mahmoud Al-Qally, Mkufunzi wa Maendeleo Endelevu.


Wengine ni Dk Ahmed Al-Rifai, Mtaalamu wa Sayansi ya Siasa, Dk Dalia Ghazlan, Mtaalamu wa Uelimishaji wa Afya, Hamada Qaoud, Mtaalamu wa Maendeleo Endelevu kutoka Taasisi ya Kitaifa ya Utawala na Maendeleo Endelevu, Ahmed Abu Douma, Mwenyekiti wa Kamati ya Kisheria ya Jukwaa la Vijana wa Kiarabu kwa Maendeleo Endelevu na Dk Rumaila Shahir, Mshauri wa Maendeleo ya Biashara na Maendeleo Endelevu na Mkuu wa Chuo cha Kijerumani  Cairo.


Pia, Mtafiti wa Anthropolojia Hassan Ghazaly, Mwanzilishi wa Mtandao wa Mshikamano wa Kimataifa na Mwanachama wa Umoja wa Waandishi wa Habari wa Afrika, alizungumzia umuhimu wa daktari kujifunza anthropolojia, ili kumsaidia kuelewa jamii zinazohitaji miradi ya maendeleo katika sekta ya afya.


Vilevile Ghazaly alielezea dhana ya diplomasia ya umma na aina zake, pamoja na fursa zinazotolewa na serikali ya Misri kwa madaktari wa Kiafrika na fursa zinazotolewa na Umoja wa Afrika kwa ajili ya kujitolea katika taasisi za kiafya barani Afrika.


Ghazaly alitoa shukrani za dhati kwa Profesa Mohy El-Din Ragab El-Banna, Mkuu wa Chuo cha Tiba na Upasuaji wa Chuo Kikuu cha Kisasa na Profesa Hisham Mohamed Omran, Naibu Mkuu wa Chuo anayeshughulikia masuala ya wanafunzi, kwa kutambua ushirikiano wao na juhudi zao katika kuwaunga mkono wanafunzi wa chuo hicho, hasa wanafunzi wa Kiafrika, na kwa juhudi zao katika kuwawezesha na kuwajumuisha katika shughuli za kitaaluma na kijamii ndani ya chuo.


Diplomasia ya vijana, diplomasia ya umma, sera za vijana za kujitolea barani Afrika, sheria ya kimataifa na afya, ujuzi wa mazungumzo na maafikiano, uuzaji binafsi wa madaktari, afya ya jamii na maendeleo endelevu, pamoja na nafasi ya vijana katika kuunda sera za afya.


Mpango huu unachukuliwa kuwa hatua ya kimkakati ya kubadilisha mwelekeo wa elimu ya tiba kutoka tu kwenye nadharia za kitaaluma hadi kuelekea uwajibikaji wa kijamii na diplomasia ya afya. Lengo lake ni kuandaa kizazi kipya cha madaktari wenye uwezo wa kushiriki na kuathiri mchakato wa uundaji wa sera za afya za baadaye nchini Misri na katika eneo la Afrika kwa ujumla.


Mpango huu unachukuliwa kuwa hatua ya kwanza ndani ya mlolongo wa mipango inayolenga kujenga uwezo wa wanafunzi wa tiba, na kufungua upeo mpana kwao kuelewa nafasi pana ya daktari katika jamii si kama mtoa huduma za afya pekee, bali pia kama kiongozi, mzungumzaji, na mtoa maamuzi katika masuala ya afya ya umma.


Waandaaji wa mpango huu wamethibitisha dhamira yao ya kuendeleza juhudi hizi na kupanua wigo wake katika matoleo yajayo, kwa ajili ya kuimarisha nafasi ya Misri katika nyanja za diplomasia ya afya na maendeleo endelevu.





No comments:

Post a Comment