CCM KUWACHUKULIA HATUA KALI WASALITI - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Tuesday, August 26, 2025

CCM KUWACHUKULIA HATUA KALI WASALITI


NA MWANDISHI WETU, KIBAHA

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani kimesema kuwa hakitasita kuchukua hatua kali kwa baadhi ya wanachama wanaokisaliti chama.


Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Katibu wa Siasa Uenezi na Mafunzo Mkoa wa Pwani David Mramba amesema kuna baadhi ya wanachama wa CCM wamekuwa wakiunga mkono watu waliokihama chama na kufanya usaliti.


Mramba alisema kuwa kuna wanachama vivuli wanaunga mkono wale waliotoka CCM na kwenda upinzani hali ambayo haitakubalika na hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.


"CCM haijatuma mwanachama yeyote kwenda chama cha upinzani na tutakaye mbaini chama kitamchukulia hatua kali za kinidhamu,"alisema Mramba.


Alisema kuwa wale wanaohama wahame lakini chama hakijamtuma mwanachama yeyote kwenda chama cha upinzani.


"Taratibu za kuwapata wagombea kwa kuanza mchakato Juni 28 mwaka huu na vikao mbalimbali hivyo taratibu zote zilifuatwa hivyo hakuna aliyeonewa,"alisema Mramba.


Aidha alisema kuwa CCM imejipanga vizuri kwenye uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na madiwani Oktoba mwaka huu kwa kuhakikisha kinapata ushindi wa kihistoria.


No comments:

Post a Comment