NA MWANDISHI WETU, KIBAHA
SHULE za Filbert Bayi za Msingi na Sekondari za Kibaha na Kimara zimeadhimisha Tamasha la michezo la miaka 13 kwa kushiriki michezo mbalimbali kwa shule hizo na shule rafiki.
Akifungua michezo hiyo kwenye Shule za Filbert Bayi Kibaha Makamu wa Rais wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) Henry Tandau amepongeza shule hiyo kwa kufanya matamasha hayo kila mwaka.
Tandau amesema kuwa matamasha hayo yanasaidia kuinua vipaji pia michezo ni ajira na ni afya katika kuimarisha wanafunzi kimasomo.
Naye Mkurugenzi wa Michezo wa shule za Filbert Bayi Cathbert Bayi amesema kuwa matamasha hayo yana lengo la kuinua vipaji ili waweze kushindana ndani na nje ya nchi.
Bayi amesema kuwa wanawajengea mazingira mazuri wachezaji wa shule hizo pia kuboresha afya na kuomba wadau mbalimbali kujitokeza kuunga mkono shule hiyo ili kuboresha matamasha hayo.
![]() |
Nao baadhi ya wanafunzi wanaoshiriki tamasha hilo wameishukuru shule hizo kwa kuandaa michezo ambayo itawasaidia kuinua vipaji vyao vya michezo mbalimbali.
Baadhi ya michezo iliyochezwa ni pamoja na mpira wa miguu, kuvuta kamba, mpira wa pete, kuvuta kamba, mbio za puto na kukimbia na magunia kwa wavulana na wasichana.
Shule zinazoshiriki tamasha hilo mbali ya zile za Filbert Bayi nyingine ni East Coast na Mwanalugali kwa upande wa Sekondari na Lulanzi na Mkuza kwa upande wa shule za Msingi.
No comments:
Post a Comment