TUCTA WAZINDUA JENGO JIPYA ARUSHA, JOWUTA YAPOKELEWA RASMI - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Saturday, August 16, 2025

TUCTA WAZINDUA JENGO JIPYA ARUSHA, JOWUTA YAPOKELEWA RASMI


NA MWANDISHI WETU, ARUSHA 


SHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania(TUCTA)limezindua jengo lake jipya katika jiji la Arusha shehehe.zilizokwenda sambamba na kutolewa vyeti kwa vyama wanachama.


 Miongoni mwa vyama 16 ambavyo vilipewa vyeti ni Chama cha Wafanyakazi wa vyombo vya Habari Tanzania(Jowuta).



Cheti hicho kimekabidhiwa na

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Ridhiwani Kikwete kwa Mwenyekiti wa Jowuta,Mussa Juma Siwayombe.


Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye hafla ya uzinduzi wa jengo la biashara la Shirikisho hilo, lililopo jijini Arusha,ambapo Ridhiwani alikuwa mgeni rasmi


Akizungumza mara baada ya mabidhiano hayo, Rais wa Tucta, Tumaini Nyamhokya, amesema kujiunga kwa Jowuta kunafanya Shirikisho hilo sasa  kuwa na jumla ya vyama 16 kutoka 13 vilivyokuwa awali.


Kutokana na hatua hiyo, Nyamhokya aliwashauri waandishi kujiunga na chama hicho ili kuendelea kupata fursa mbalimbali zikiwemo kutetewa maslahi yao na elimu kuhusiana na masuala yanayohusu kazi.


Rais huyo amesema ukiacha Jowuta, Vyama vingine vipya vilivyopewa vyeti ni Chama cha Wafanyakazi sekta ya Ulinzi Binafsi(Tupse), na Chama cha wafanyakazi wa Huduma za Viwandani Tanzania(Tasiwu).


Akizungumzia hatua hiyo,Mwenyekiti wa Jowuta, Musa Juma amesema wanashukuru TUCTA kuwapokea na kuwapa cheti rasmi.



Amesema kwa sasa kazi iliyombele yao Viongozi wa JOWUTA ni kutetea maslahi na mazingira.bora ya kazi kwa wanahabari.


"Tutashirikiana na viongozi wengine wa TUCTA kusaidia wanahabari kufanyakazi kwa kuzingatia sheria ikiwepo wanahabari kuwa.na ajira na mikataba inayotambulika kusheria"alusema


Kwa upande wake Waziri Ridhiwani,amesema Shirikisho la vyama vya wafanyakazi lina umuhimu na historia kubwa katika nchi hii kabla ,wakati na baada ya uhuru.


"Ambaye haoni kama shirikisho hilo lina umuhimu katika nchi hii, huyo hatakuwa mzalendo.


"Pia hata mafanikio yote ambayo serikali inajivunia leo huwezi kuacha kuwataja wafanyakazi ikiwemo mafanikio katika sekta ya elimu, ujenzi wa SGR au mafanikio ya bandari, kwa hiyo muelewe hakuna siku serikali itawadharau na kuwasahau wafanyakazi,"amesema Ridhiwani.


Uzinduzi wa Jengo


Kuhusu jengo lililozinduliwa,  Waziri huyo amesema imeonyesha namna vyama hivyo vimeamua kuunga mkono serikali katika uchumi na maendeleo ya kijamii kwa kuwa halitakuwa tu na faida kwa TUCTA bali kuchangia ukusanyaji kodi. 


"Uwekezaji katika jengo hili unasaidia kataka kukuza ustawi wenu na utoaji huduma kwa jamii.


"Hivyo nitoe  rai kwenu Tucta kulitumia jengo hili katika kuendeleza mshikamano kwa kuwa kwa kufanya hivyo mtajenga taasisi iliyo imara na kuzidi kuaminiwa na serikali.


Awali akizungumzia mradi huo, Rais wa Tucta,Nyamhokya amesema jengo hilo lilianza kujengwa miaka ya 1975 miaka ya 90 jengo hili likamaliziwa kwa kuingia mkataba na wafanyabiashara kujenga vibanda.


Hata hivyo ujenzi wa awamu huo,ulifanyika kuanzia mwaka 2023 na jengo  limemalizika kwa asilimia 98 nalina jumla ya wapangaji 113 ambapo litawezesha kuiingizia TUCTA mapato ya Sh50 milioni kwa mwezi.


"Mbali na vyumba vya biashara pia jengo hili lina hoteli na chumba maalum(Presidental suit),"amesema Nyamhokya.


No comments:

Post a Comment