NA MWANDISHI WETU
MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Chamazi jijini Dar es Salaam, kupitia Chama Cha Wananchi (CUF) Said Mng’agi, amesema ikiwa atachaguliwa kuwa mbunge atahakikisha kodi zote zisizokuwa za msingi zinaondolewa ili kutoa fursa ya kuwapunguzia mzigo wananchi wakiwemo wafanyabiashara.
”Tanzania hii inautajiri mkubwa wa vyanzo vya kukusanya mapato bila kumgusa mwananchi wa kawaida ambaye kula kwake inategemea kipato chake kwa siku hususan wanaofana biashara ndogondogo, hivyo mkinichagua nitakwenda kupeleka hojqa bungeni kuhakikisha kodi kandamizi zinaondolewa,” amesema.
Hayo ameyasema leo Septemba 25 , 2025 katika kampeni za kusaka kura kwa wananchi wa jimbo hilo aliyoifanya katika eneo la Chamazi Magengeni, ambapo pia aliwahakikishia wananchi hao kuwa ikiwa atachaguliwa kuwa mbunge atalisemea ipasavo sula la tozo ya kuchukua maiti hospitlini ziondolewe.
Amefafanua kuwa suala la kuzuia maiti inaofanywa na hospitali nyingi hapa nchini si kitendo cha kiungwani kutokana na kwamba kinazidisha majozi kwa wafiwa, kwa maana ndugu wanapofiwa wanahitaji kuchangiwa michango ili waende kumsitiri ndugu yao, inapokuja suala la kuzuia mwili hadi ilipwe fedha inawapa machungu na mzigo mkubwa.
Kutokana na kuwepo changamoto hiyo amewaahidi wananchi wa jimbo hilo ikiwa atakuwa mbunge atakwenda bungeni kulisemea kwa nguvu zote ili tozo hiyo iondolewe kabisa na si kupewa maiti na kuambiwa waje kulipa deni baadaye.
Pia amewataka wananchi hao kuwahoji wagombea ubunge wanaokwenda hapo kuomba kura hususan wa CCM kwamba katika kipindi kilichopita wanawafanyia nini wakazi hao ili waweze tena kuwapigia kura ili washinde kwenye uchaguzi ujao.
Naye Mwenyekiti wa chama hicho Wilaya ya Temeke, Seif Kopi, ametoa wito kwa vijana na makundi mengine kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi kukipigia kura Chama Cha Cuf, ili kipate ushindi wa kuongoza jimbo hilo kwa miaka mitano ijayo.
“Vijana wangu na makundi mengine mkiwemo akina mama msifanye makosa Oktoba 29, jitokezeni kwa wingi kuja kutuchagua kuanzia Udiwani, Ubunge na Urais jambo litakalosaidia kuja kuondoa changamoto nyingi ambazo chama tawala kimeshindwa kuziondoa tangu uhuru,” amesema.
Pia Mwenyekiti wa Jumuia ya Wanawake wa Chama hicho Wilaya ya Temeke Jamila Kudimba, amesema huu ndio wakati wa wananchi wa Chamazi kutofanya makosa katika Uchaguzi Mkuu ujao, wanachatakiwa ni kufanya mabadiliko kwa kukipigia kura Cuf ili kiweza kuleta maendelea katika Jimbo hilo.
“Nawaombeni wananchi wa jimbo hili msifanye makosa Oktoba 29, jitokezeni kwa wingi na mkichague chama cha CUF kwa kuwapigia kura kwa wingi kwa wagombea wetu ili walete mabadiliko ya kweli na kuleta ahadi za uongo kama wengine ambao wametawala kwa kipindi kirefu, “amesema
.
No comments:
Post a Comment