RAIS SAMIA KUANZA UTEKELEZAJI WA BIMA YA AFYA KWA WOTE NDANI YA SIKU 100-JENISTA MHAGAMA - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Monday, September 29, 2025

RAIS SAMIA KUANZA UTEKELEZAJI WA BIMA YA AFYA KWA WOTE NDANI YA SIKU 100-JENISTA MHAGAMA


NA MWANDISHI WETU

MGOMBEA Ubunge Jimbo la Peramiho Bi. Jenista Mhagama amesema kuwa Mgombea nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ataanza mara moja utekelezaji wa Sheria ya Bima ya Afya kwa wote ndani ya Siku 100, baada ya kuteuliwa kuwa Rais. 


Amesema hayo Septemba 28 2025 akiwa katika Kijiji cha Lyangweni Kata ya Litapwasi katika Wilaya ya Songea Vijijini wakati wa Kampeni za kunadi Sera za Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuwaomba wananchi kuipigia kura za ndio CCM katika uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025.


“Mgombea urais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema ndani ya siku 100 yupo tayari kutoa huduma muhimu za matibabu kwa wazee, akina mama wajawazito na Watoto kupitia bima ya afya kwa wote, kwa hiyo wazee mna fungu lenu kwa kupitia Bima ya Afya kwa Wote ili muweze kukabiliana na matatizo ya afya,” amesema Mhagama. 


Mhagama amesema kuwa Rais Samia anajua kuwa Watanzania wengi wanasumbuliwa na magonjwa yasiyoambukiza yakiwemo presha, kisukari na saratani na matibabu ya magonjwa hayo yana gharama kubwa ambazo watanzania wengi hawana uwezo wa kumudu gharama za vipimo na matibabu.


“Mgombea wetu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema watanzania watakaougua magonjwa alafu watakuwa hawana uwezo, Serikali itasimia gharama za vipimo na matibabu yao,” amesema Bi. Mhagama na kuwaomba wananchi kujitokeza Oktoba 29, 2025 na kukipigia kura za ndio Chama Cha Mapinduzi (CCM).




No comments:

Post a Comment