DKT. BITEKO AWATAKA CCM USHIROMBO KUSHIKAMANA - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Monday, September 29, 2025

DKT. BITEKO AWATAKA CCM USHIROMBO KUSHIKAMANA


NA MWANDISHI WETU

MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Bukombe kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Doto Mashaka Biteko amewataka wanachama wa CCM Kata ya Ushirombo Wilayani Bukombe kushirikiana na kushirikiana ili kujiletea maendeleo.


Amesema hayo Septemba 29, 2025 wakati akihuhutubia mkutano wa kampeni katika Kata ya Ushirombo wilayani Bukombe mkoani Geita ikiwa ni sehemu Kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani utakaofanyika Oktoba 29, mwaka huu.


“ Nataka niwaambie wana CCM siri ya ushindi ni umoja, wana CCM wa Ushirombo tuungane,  twende pamoja, tushikamane ili tujiletee maendeleo,” amesema Dkt. Biteko.


Ameendelea  kuwahimiza wanachi hao kuishi kama ndugu, kuvumiliana na kusameheana ikitokea wakahitilafiana  “Wakati Mungu amekupa maisha ya kuwa duniani ishi na watu vizuri kwa sababu kuna wakati utamhitaji mtu pendaneni na mshirikiane, na kama mmekoseana sameheaneni ”


Sambamba na hayo Dkt. Biteko amesema kuwa maendeleo yote yaliyopatikana katika Kata hiyo ikiwemo miradi ya maji, mikopo kwa vikundi vidogo vidogo, ujenzi wa shule, barabara na umeme yametokana na ushirikiano miongoni mwa wananchi wa kata hiyo na hivyo kuwahimiza kuendeleza ushirikiano huo kwa maendeleo zaidi ya baadaye.


Ameongeza kuwa Kata hiyo ina shule mbili za sekondari Mwalo na zingine zitajengwa Ishikaibuda na Ilyamchele.


“ Tuna zahanati mbili na tunataka tujenge nyingine mbili na kati ya hizo moja itakuwa kituo cha afya. Nataka niwaombe watu wa Kata ya Ushirombo ili tufanikiwe siri ni moja tu ushirikiano,” amesisitiza Dkt. Biteko.


Aidha, amesema  Dkt. Samia Suluhu Hassan amedhamiria kuona Bukombe ikibadilika ndio maana wanajenga viwanja vya michezo, barabara za lami na jengo la halmashauri.


Hivyo, amewaomba wananchi hao Oktoba 29 wamchague  Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Doto Mashaka Biteko kuwa mbunge wa Bukombe pamoja na Lameck Warangi kuwa diwani wa Kata ya Ushirombo.


Kwa upande wake Mgombea wa Udiwani Kata ya Ushirombo, Lameck Warangi amesema katika kipindi cha mwaka 2020/2025 Wananchi wa Kata hiyo wamefusiri na kutekeleza  Ilani ya CCM kwa kujenga na kusimamia miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa shule, miradi ya maji na miundombinu ya umeme.


“ Hatukuwa na miradi ya maji na sasa tunayo, tuna shule mbili za sekondari, ninyi ni mashahidi leo tuna umeme kila kijiji hizo ni hatua jubwa na ipo sababu kubwa ya kuipa CCM kura za kutosha,” amesema Warangi


Amenasibisha mafanikio yaliyopatikana na uongozi madhibuti na usimamizi thabiti wa Rais Samia na hivyo kuwaomba wananchi kumpa kura nyingi za ndiyo ili kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya maendeleo ya Kata, Wilaya na Taifa kwa ujumla. 


“Dkt.  Samia anajua mahitaji ya Kata yetu  ikiwemo kupanua usambazaji wa maji, kufikisha umeme katika vitongoji na ukamilishaji wa zahanati hivyo wampigie kura Oktoba 29, 2025 ili aweze kukamikisha miradi hiyo.




No comments:

Post a Comment