RIDHIWANI KIKWETE AAHIDI KUSIMAMIA UPATIKANAJI WA MBOLEA YA RUZUKU - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Monday, September 22, 2025

RIDHIWANI KIKWETE AAHIDI KUSIMAMIA UPATIKANAJI WA MBOLEA YA RUZUKU


NA MWANDISHI WETU, PWANI


 MGOMBEA Ubunge wa Chama Cha Mapinduzu (CCM) Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete amesema kuwa moja ya mambo atakayoyasimamia ni uendelevu wa upatikanaji wa mbole ya ruzuku.


Kikwete ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa kampeni kwenye kata ya Kiwangwa na kumnadi mgombea udiwani wa Kata hiyo Malota Kwaga.


Amesema kuwa mbolea ya ruzuku ni moja ya vitu muhimu kwa wakulima kwani inawapunguzia gharama za kilimo hivyo lazima lisimamiwe vizuri ili ipatikane kwa wakati.


"Jambo lingine ambalo nitalisimamia ni kuhakikisha mbolea ya ruzuku inapatikana kwa uhakika ili muweze kuendeleza kilimo chenu cha nanasi ambalo ndiyo zao kuu la biashara kwenye Kata yenu,"amesema Kikwete.


Aidha amesema upatikanaji wa pembejeo za kilimo ni kipaumbele kwa wakulima hasa ikizingatiwa Kiwangwa ni moja ya maeneo yenye kilimo kikubwa cha zao la nanasi.


"Naomba ikifika Oktoba wapigieni kura za kutosha Mgombea wetu wa Urais Dk Samia Suluhu Hassan, mimi niwe Mbunge wenu na Diwani wote tunaotokana na CCM tutaendeleza maendeleo yaliyopatikana ili tupige hatua zaidi,"amesema Kikwete.


Naye Mgombea Udiwani Kata ya Kiwangwa Malota Kwaga amesema kuwa kutokana na upatikanaji mbolea ya ruzuku mananasi yanalimwa mwaka mzima hivyo kipaumbele hicho lazima akipambanie atakapoingia pale Halmashauri.


Kwaga amesema kuwa atasimamia upatikanaji pembejeo za kilimo ili wakulima wapate urahisi wa upatikanaji wa mahitaji muhimu ya kilimo kikiwemo cha nanasi ambacho ni zao la kiuchumi kwa wananchi wa Kiwangwa.



No comments:

Post a Comment