RUVUMA CHANGAMKIENI HUDUMA ZA KIBINGWA ZA MADAKTARI BINGWA WA RAIS SAMIA- MHAGAMA - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Monday, September 22, 2025

RUVUMA CHANGAMKIENI HUDUMA ZA KIBINGWA ZA MADAKTARI BINGWA WA RAIS SAMIA- MHAGAMA


NA WAF, RUVUMA

TIMU ya madakatari bingwa wapatao 50 wa Dkt. Samia Suluhu mapema leo Septemba 22, 2025 wamepokelewa na mkoani Ruvuma na Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama ikiwa ni muendelezo wa utoaji huduma za Mkoba zinazowafuata wananchi kwenye maeneo yao, sambamba na kuwajengea uwezo wataalam wa afya ngazi ya msingi. 


Huduma  hiyo ya Madaktari bingwa wa Rais Samia inatarajiwa kutoa huduma katika Halmashauri zote nane(8) za mkoa wa Ruvuma kwa muda wa siku tano zikijumuisha huduma za magonjwa ya wanawake na ukunga, watoto wachanga, upasuaji, mfumo wa mkojo, usingizi na ganzi salama, magonjwa ya ndani, afya ya kinywa na meno pamoja na koo pua na masikio.


Waziri Mhagama mbali ya kuwakaribisha mkoani hapo na kuwasihi Mabingwa hao kufanya kazi yao kwa kuzingatia miiko na maadili ya kazi, vilevile amewaomba wananchi wa mkoa wa Ruvuma kwenye Halmashauri zote kujitokeza kwa wingi ili  kupata huduma za uchunguzi na ushauri wa kitabibu.


Hospitali zote za halmashauri ndani ya mkoa, zitahisika kwenye kambi hiyo ya siku tano (5)  katika halmashauri Saba (7) na manispaa moja ya Songea halmashauri hizo ni pamoja na Nyasa,Tunduru, Mbinga, Namtumbo, Madaba,  Mbinga Songea Mji na Mbinga Mji, ambazo zote zitapokea jozi madaktari bingwa watano (5) pamoja na muuguzi bingwa mmoja na katika hospitali ya Manispaa ya Songea itapokea jozi  ya madakari bingwa nane (8).


Wakati wa mapokezi hayo Waziri Mhagama aliambatana na Katibu tawala wa mkoa huo Mary Makondo.




No comments:

Post a Comment