NA MWANDISHI WETU
CHAMA Cha African Democratic Alliance Party (ADA TADEA), kimesema kwamba kikifanikiwa kuingia madarakani katika uchaguzi Mkuu ujao, Serikali watakayounda wataanza na Mapinduzi ya kichumi.
Hayo yamebainishwa leo Septemba 14, 2025 jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa kampeni za mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzanja kupitia chama hicho, Georges Busungu.
"Tukichaguliwa kuingia madarakani tutajipanga na mchakato wa kukuza uchumi kuwa kubadilisha fikra za wananchi WETU kupitia nyanja ya Kilimo, ufugaji, utalii na kuwajengea uwezo wa kitaaluma," amesema.
Amefafanua kuwa Mtanzania ukimjenga vema katika fikra yakinifu ataweza kijikwamua kichumi kupitia nyanja hizo na kupata mafanikio na kuondoka na umasikini ujinga na maradhi.
Aliweka wazi kuwa katika taaluma, elimu itatolewa bure kuanzia ngazi ya awali hadi Chuo Kikuu na wanafunzi wataongezewa somo la kujitegemea itakayosaidia baada ya masomo kuwa na uwezo wa kijiajiri na kukimbilia kwenye Vyuo vya Ufundi kutafuta ujuzi.
Pia ameongeza kuwa wataalamu wa kitanzania ambao wanafanya kazi nje ya ikiwemo Marekani watarudishwa hapa nchini ili waendeleze ujuzi wao kwa Watanzania.
Aidha, amedadavua kwamba pindi atapoingia madarakani, Serikali atakayounda haitaangalia chama bali uwezo wa mtu ili kuleta maendeleo kwa pamoja huku wakitengeneza katiba bora, itakayonufaisha wananchi.
Naye Mwenyekiti wa Chama hicho ambaye ni Mgombea Urais kwa tiketi ya chama hicho katika Serikali ya Zanzibar,Juma Alli Khatib, amesema ikiwa, Busungu atachaguliwa kuwa Rais, akina mama watakaojifungua watapewa maziwa ya kopo mwa miezi miwili ili kujenga afya ya mtoto.
Picha zote Kwa Hisani ya TBC
No comments:
Post a Comment