NA MWANDISHI WETU
HaloPesa imehitimisha rasmi kampeni yake ya “Tamba na Bonasi” kwa mafanikio makubwa, baada ya kuwazawadia maelfu ya wateja wake zawadi na bonasi mbalimbali zenye thamani kubwa, ikiwemo fedha taslimu hadi Shilingi Milioni Mbili (2,000,000) zilizokuwa zikitolewa kila siku, kila wiki na kila mwezi.
Katika kilele cha kampeni hiyo, mmoja wa washindi wakubwa kutoka Zanzibar alikabidhiwa hundi ya Shilingi Milioni Mbili (2,000,000) katika hafla iliyofanyika katika duka la Halotel lililopo Michenzani Mall, Zanzibar, tukio lililovutia wateja na wadau mbalimbali wa huduma za kifedha kidijitali.
Hafla ya makabidhiano iliongozwa na Mkurugenzi wa Biashara wa Halotel Tawi la Zanzibar, Bw. Aboubakari Ngatomela, akishirikiana na Afisa Biashara Zanzibar, Hajjy Khamis Hajji, huku wateja wakishuhudia tukio hilo kama ishara ya uwazi na uhalisia wa zawadi zinazotolewa kupitia kampeni ya Tamba na Bonasi.
Kupitia kampeni hiyo, wateja wa HaloPesa walipata nafasi ya kushinda bonasi kila walipofanya miamala yao ya kila siku, ikiwemo kutuma na kutoa pesa, kulipa bili pamoja na kununua bidhaa na huduma mbalimbali kupitia mfumo wa HaloPesa.
Kampeni ya “Tamba na Bonasi” ililenga kuhamasisha matumizi ya huduma za kifedha kidijitali sambamba na kuwashukuru wateja kwa kuendelea kuiamini HaloPesa, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 9 ya HaloPesa na miaka 10 ya mtandao wa Halotel nchini Tanzania.
Akizungumza kuhusu mafanikio ya kampeni hiyo, Meneja Masoko wa HaloPesa, Aidat Lwiza, alisema kampeni hiyo imeimarisha mahusiano kati ya HaloPesa na wateja wake kote nchini, huku maelfu ya wateja wakinufaika na bonasi na zawadi mbalimbali.
Aliongeza kuwa HaloPesa itaendelea kuboresha huduma zake kwa kutoa makato nafuu zaidi, kuimarisha mifumo ya kidijitali na kuendelea kubuni ofa na promosheni zitakazoongeza thamani na kurahisisha miamala ya kifedha kwa wateja wake.
Kwa kuhitimisha kampeni hiyo, HaloPesa imewaahidi wateja wake kuendelea kuwapatia huduma bora zaidi mwaka 2026, huku ikiwatakia Heri ya Mwaka Mpya na kuwakumbusha kuwa mawasiliano rasmi kutoka HaloPesa na Halotel hufanyika kupitia namba 100 pekee.
.png)
.png)




No comments:
Post a Comment