NA MWANDISHI WETU
MWENYEKITI wa Chama Cha Wananchi (CUF)Taifa,Prof. Ibrahim Lipumba, amewasihi Watanzania wasikubali kubaguliwa kwa misingi ya dini, Utanganyika na Uzanzibar.
Prof Lipumba amebainisha hayo leo, Januari 27, 2026 wakati wa kuwaombea wanachama wao waliokufa wakati wa maandamano yaliyofanyika Pemba na Unguja, Zanzibar Januari 27, 2001.
Dua hiyo inafanyika ikiwa ni miaka 25 imepita tangu maandamano hayo kufanyika, visiwani humo baada ya Uchaguzi Mkuu kufanyika Oktoba mwaka 2000 ambapo Prof. Lipumba ameongeza kuwa,
" Watanzania tusikubali agenda ya kubaguana kwa misingi ya kidini, kisiasa ama Utanganyika na Uzanzibari kwani Tanzania ikiharibika wote tumeharibikiwa", amesema.
Amesisitiza kuwa matatizo yanapotokea katika nchi ni vema yakatatuliwa kwa amani na utulivu ili kuendelea kudumu katika misingi ya haki na utulivu na si vinginevyo.
Prof. Lipumba amefafanua kuwa sio kweli wanaosema kwamba yaliyojitokeza wakati wa uchaguzi Mkuu 2025 na 2001 ni kutokana na udini bali ni masuala ya kukosekana kwa haki kutokana na kutangazwa washindi kwa baadhi ya wasiochagukiwa na Wananchi na si vinginevyo.





No comments:
Post a Comment