RAIS DKT SAMIA AWAKIMBILIA WENYE UHITAJI SHULE YA MSINGI MAZINYUNGU KILOSA - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Tuesday, January 27, 2026

RAIS DKT SAMIA AWAKIMBILIA WENYE UHITAJI SHULE YA MSINGI MAZINYUNGU KILOSA


NA MWANDISHI WETU

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa zawadi kwa wanafunzi wenye uhitaji maalum katika shule ya Msingi Mazinyungu, Wilayani Kilosa ikiwa ni sehemu ya tukio la kumbukizi ya siku ya kuzaliwa Januari 27, 2026.


Zawadi hizo zilizokabidhiwa na Mkuu wa Wilaya  Kilosa Shaka Hamdu Shaka ni pamoja na Magodoro, Mashuka,Vyandarua, Sabuni za kufuli na kuogea, Mafuta maalum kwa wenye ulemavu wa ngozi pamoja na Chakula.


Tukio hilo adhimu ni sehemu ya kumbukizi ya siku ya kuzaliwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia  Suluhu Hassan alizaliwa tarehe 27 Januari, 1960 katika Kijiji cha Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar. 


Watoto hao wenye uhitaji maalum pia  walikata keki ikiwa ni ishara ya kuungana na Mhe Rais Samia  katika siku yake hii kwenye safari ya maisha yake

No comments:

Post a Comment