* Viongozi Serikali za Mitaa nao kuswekwa ndani
NA MWANDISHI WETU
MKUU wa Wilaya ya Ubungo, Albert Msando ametoa maelekezi kwa Wakala wa Barabara Mijini na Vijini, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), kwamba kabla ya kuanza ujenzi wa barabara, usambazaji umeme wawashirishe Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ili kufanikisha kuyafikia majanga ya moto kwa urahisi pindi yanapotokea.
Pia amewataka ametoa maelekezo kwa Jeshi hilo, kushirikiana na Shirika la Viwango Tanzania (TBS), kuvifanyia ukaguzi wa vifaa vya umeme ambavyo vimetumika kuunganisha umeme kwenye masoko na maduka.
Amesema jeshi hilo na TBS wanatakiwa kufanya ukaguzi huo ili kubaini ubora wa vifaa na kama itabainika kuwa ni hafifu, aliyeunganisha umeme na mmiliki wachukuliwe hatua za kisheria.
"Jeshi la Zimamoto ni wakaguzi hivyo shirikianeni na TBS ili kubaini vifaa vilivyofungwa kwenye maduka, na masoko ili kuona kama vina ubora stahiki au la ukiwa tofauti wahusika wachukuliwe hatua za kisheria," amesema.
Aidha akifafanua kuhusu Tarura, amesema haitakuwa Jambo la busara kufanya ujenzi pasipo kuwashirisha Zimamoto kwani kinachotakiwa magari ya Zimamoto wanapokwenda kwenye majanga ya moto yaweze kufika na kugeuza kwa urahisi.
Amesisitiza kuwa hata viongozi wa Mtaa wakaofumbia macho barabara kujengwa kwa ufinyu na kusababisha magari ya Zimamoto kushindwa kufika kwa urahisi panapotokea majanga ya moto nao watakuwa kikaangoni.
"Nitawaweka ndani, viongozi wa Serikali za Mtaa watakaofumbia macho ujenzi hafifu wa barabara usiozingatia athari za moto na hivi karibuni nitafanya ziara Sinza kuangalia kama zinaviwango vya Jeshi la Zimamoto,' amesema.
Wakili Msonda, alitoa maelekezo jana akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila ametoa jana wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Zimamoto Duniani yalifanyika jijini humo.
Kwa upande wake Naibu Kamishna wa Zimamoto na Uokoaji Tanzania na msemaji wa jeshi hilo DCP Puyo Nzalayaimisi ameishukuru Serikali kwa kulipatia magari na vifaa vya kisasa kwa ajili ya kuzimia mioto na kufanya Uokoaji pindi majanga yanapotokea.
"Tunashukuru sana Serikali ya Dkt.Samia Sululu Hassan kwa kuliborsha Jeshi letu kwa kutupatia vifaa vya kisasa,na sisi tunaendelea kujitoa kwa moyo wa dhati katika kuwahudumia Wananchi"amesema.
Awali Kamanda wa Jeshi hilo Mkoa wa Kizimamoto Ilala SACF Mabusi Peter amesema kuwa sasa wapo kwenye mchakato wa kufungua vituo vingine vinne vya Zimamoto katika maeneo ya Kinyerezi,Kivule,Masaki na Kigamboni.
Pia amesema kuwa jeshi hilo linaendelea kushirikisha wadau pamoja na kutoa elimu kwa wananchi nakwamba kwasasa jeshi hilo lina wadau wa kujitolea wapatao 75, pia klabu 50 zenye wanachama 1000.





No comments:
Post a Comment