- MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Tuesday, May 29, 2012

Five Star kufanya kweli Panandi Panandi leo

Na Hamisi Magendela
KUNDI la muziki wa taarabu nchini Five Star Modern linatarajiwa kufanya onesho la kukata na nashoka katika ukumbi wao wa nyumbani wa Panandi Panandi ili kukonga nyoyo za mashabiki wake wa eneo hilo la Ilala na vitongoji vyake.

Rais wa kundi la Five Star Modern Taarabu Alli Juma 'Alli Jay 'kushoto akizungumza katika moja ya mikutano yake na waandishi wa habari.
 Akizungumza na Jambo leo Dar es Salaam jana, rais wa kundi hilo Alli Juma 'Alli Jay' alisema wamejipanga kufanya onesho hilo kesho katika ukumbi huo wa Panandi Panandi Ilala Dar es Salaam ili kukonga nyoyo za mashabiki wao ambao siku zote walikuwa wakiambulia kushuhudia mazoezi pekee.
"Kesho tutakuwa katika Ukumbi wa Panandi Panandi Ilala Dar es Salaam kutoa burudani kwa mashabiki wetu wa nyumbani ambao kila siku walikuwa wakishihudia mazoezi yetu pekee na raha kwenda kuwapa wengine," alisema Alli Jay.
Pia alisema Juni 8 wanatarajia kwenda kutoa burudani katika Ukumbi wa Mapinga, Bagamoyo mkoani Pwani ambapo wanatarajiwa kuwaburudisha vya kutosha wakazi wa huko.
Alli Jay alisema siku inayofuata watakuwa kwenye Ukumbi wa Mawenzi Garden Tabata Dar es Salaam ambapo pia watatoa burudani ya uhakika kwa nyimbo mpya na za zamani ambayo zinatikisa katika maoeneo mbalimbali ya Tanzania na viunga vyake.


Aliyetimuliwa Twanga aula Mashujaa
Na Mwandishi Wetu
ALIYEKUWA Meneja wa Masoko bendi ya African Stars 'Twanga Pepeta', Martine Sospeter, ametangaza rasmi kujiunga katika bendi ya Mashujaa Musica.
Akizungumza Dar es Salaam jana katika mkutano na waandishi wa habari, Sospeter, alisema uamuzi huo umekuja baada ya kuona hakutendewa haki na mwajiri wake katika bendi ya Twanga Pepeta.
Alisema mwishoni mwa wiki iliyopita alishangazwa na kauli ya Mkurugenzi wa Twanga Pepeta, Asha Baraka, kutangaza katika vyombo vya habari kuwa amemfukuza kazi kutokana na kuihujumu bendi yake, ikiwemo kushawishi wanamuziki kujiunga na bendi ya Mashujaa Musica.
"Kwa kweli kauli ile ilinisikitisha sana kutokana na ukweli kwamba Asha nilimchukulia kama zaidi ya dada yangu, kwani nilifanya naye kazi kwa  miaka 14, iweje hii leo aje anitolee maneno ya kunichafua katika vyombo vya habari wakati kuna ofisi," alisema Sospeter.
Alisema hajawahi kuhusika na mpango wowote wa wasanii wa Twanga kuhamia Mashujaa Musica, na wala hakuwa anafahamu mpango huo zaidi ya mwisho wa siku kusikia fununu za chini chini kabla ya kuhamia Mashujaa.
Mbali na mkataba, baadhi ya makubaliano na uongozi wa Mashujaa ni pamoja na kumpangia nyumba, hali iliyomlazimu kuhama Twanga.
Alisema anaamini atafanya vyema kazi yake mpya kama ilivyokuwa Twanga, ambapo alidumu kwa muda mrefu na kuchangia kufika alipoiacha, na kuomba ushirikiano kwa uongozi, wanamuziki, wadau na hata na waandishi wa habari.
Martine, ametambulishwa asubuhi hii katika mgahawa wa Business Park, Victoria, Dar es Salaam. Pamoja na utambulisho huo, pia Martine amekanusha madai ya Mkurugenzi wa Twanga Pepeta, Asha Baraka kwamba ametoweka na fedha za bendi hiyo.
Katika taarifa yake ya kumfukuza kazi Martine, Asha alidai Meneja huyo alichukua fedha kwa wateja kwa ajili kuwakodisha bendi- hivyo akamtaka azirejeshe. “Sijachukua fedha yoyote popote, sina deni, kama anadai nina deni, alete ushahidi,”alisema Martine.
Sospeter, alisema kwa muda mrefu amekuwa akitakiwa na bendi ya Mashujaa kwa dau zuri, lakini amekuwa akikataa kutokana na jinsi anavyomheshimu Asha Baraka, lakini amesikitishwa kwa kufukuzwa kwa kudhalilishwa.
"Amenikfukuza na kunitolea maneno ya kashfa wakati nipo na bendi yake ziarani mikoani, imeniuma sana. Ila bado nitaendelea kumheshimu (Asha Baraka) kama dada yangu na mtu ambaye amenifikisha hapa," aliongeza meneja huyo.
Sababu kubwa aliyoitaja Baraka ya kumfukuza Sospeter ni kuwarubuni wanamuziki wa Twanga Pepeta kuhamia kwa wapinzani wao Mashujaa.
Miongoni mwa wanamuziki wa Twanga waliohamia Mashujaa ni mwimbaji hodari, Charles Gabriel 'Chalz Baba' na mnenguaji Lilian 'Internet' Tungaraza.

Osiah naye ajivua uongozi Yanga
Na Asha Kigundula
KATIBU Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Angetile Osiah, jana ameandika barua ya kujiuzulu nafasi ya ujumbe katika Kamati ya Uchaguzi ya klabu ya Yanga.
Angetile Osiah, Katibu Mkuu wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania 'TFF' ambaye alikuwa mjumbe wa kamati ya Uchaguzi wa klabu ya soka ya Yanga ambapo ametanga kujiuzulu nafasi hiyo Dar es Salaam jana.
Kujitoa kwa Osiah kunakuja siku chache baada ya kujiuzulu kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Yanga, Lloyd Nchunga, ambaye naye alikuwa nyuma ya wajumbe zaidi ya saba wa Kamati ya Utendaji kujiuzulu kutokana na mgogoro uliokuwa ukiikumba klabu hiyo.
Hali hiyo ya kujiuzulu kwa baadhi ya viongozi ilikuwa ikishinikizwa na Baraza la Wazee pamoja na baadhi ya wanachama ambao waliutaja uongozi huo uliokuwa chini ya Nchunga kushindwa kutimiza majukumu yao ipasavyo.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Osiah, alisema ameamua kujiuzulu wafidha huo kutokana na yeye kuwa kiongozi wa TFF, hivyo hawezi kuwepo katika kamati hiyo.
Osiah, alisema ataiwahisha barua yake kwa Katibu Mku wa Yanga, Mwesigwa Selestine, kumjulisha kushindwa kwake kutumia nafasi hiyo kama alivyochaguliwa awali.
Alisema yeye ni mwanachama wa Yanga, na ataendelea kuwa mwanachana na si kuwa mjumbe wa kamati yoyote katika klabu hiyo kutokana na majukumu ya TFF.
Osiah alisema alitakiwa aachie nafasi hiyo mara baada ya kuajiriwa na TFF, lakini mambo yalikuwa mengi ambapo sasa klabu hiyo inatarajia kufanya uchaguzi wake naye hataweza kukalia kiti cha ujumbe wakati yupo katika tasisi baba ya Yanga.
"Siwezi kuendelea na wadhifa wangu wa Yanga, hivyo nimeachia ngazi nafasi hiyo na ninawasilisha barua yangu leo (jana) kwa uongozi wa Yanga ambao upo chini ya Katibu Mkuu, Selestine (Mwesigwa)," alisema Osiah.
Osiah anakuwa mjumbe wa kwanza wa Kamati ya Uchaguzi ya Yanga kutangaza kujitoa, ingawa sababu zake zinaonekana kuwa za kikatiba zaidi kwa kubanwa na majuku ya TFF.

No comments:

Post a Comment