- MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Sunday, May 27, 2012

Stars yashindwa kutamba nyumbani
*Yatoka suluhu na Malawi
*Kazi ipo kwa Ivory Coast
Na Asha Kigundula
TIMU ya soka ya Taifa 'Taifa Stars' imeshindwa kufanya vyema katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliochezwa Uwanja wa Taifa Dar es Salaam baada ya kutoka sare ya 0-0 na Malawi 'The Flame'.
Katika mchezo huo timu zote zilianza kwa kushambuliana kwa zamu huku The Flame ikionesha uhai zaidi na kuwapa kazi kubwa mabeki wa Taifa Stars  kuokoa mabao ya wazi.
Dakika ya tatu ya kipindi cha kwanza Frank Domaya nusura aipatie Malawi bao la kuongoza lakini umakini wa mchezaji Haruna Moshi 'Boban' ulifanikisha kuokoa hatari hiyo.
Katika dakika hizo za mwanzo endapo washambuliaji wa timu ya Malawi wangekuwa makini wangeweza kupata mabao ya mapema kwani dakika ya 11 mlinda mlango wa Stars Juma Kaseja aliokoa mpira uliopigwa na Frank Banda.
Malawi walizidi kuliandama lango la Stars na kuwaweka katika hali ngumu mabeki wa timu hiyo na dakika ya 33 kwa mara nyingine Frank Banda  aliikosesha timu yake bao baada ya shuti lake kuokolewa na beki, Aggrey Morris.
Hadi dakika 45 ya kipindi cha kwanza kumalizika timu hizo zilitoka uwanjani zikiwa nguvu sawa licha ya kosakosa nyingi za washambuliaji ambao kama wengekuwa makini matokeo yangekuwa tofauti.
Kipindi cha pili kilianza kwa Stars inayodhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya Kilimanjaro Premium Lager kuonesha dhahiri iko nyumbani baada ya kuonesha kandanda safi huku ikishangiliwa na umati wa mashabiki walioudhuria uwanjani hapo.
Dakika ya 58 Haruna Moshi 'Boban' aliikosesha Stars bao la kuongoza baada ya kumalizia vibaya mgongeo wa mchezaji Mbwana Samatta na kuokolewa na mabeki wa Malawi.
Wakati dakika zikizidi kuyoyoma Stars walionekana kuzinduka huku wakishangiliwa na umati mkubwa wa mashabiki waliojitokeza kuishangilia timu yao, dakika ya 86 alikosa bao baada ya shuti lake kutoka nje ya goli akiwa akiwa sentimeta chache.
Dakika 90 za mchezo huo wa kimataifa huku timu zote zikitoka suluhu ikiwa ni mchezo wa kwanza wa majaribio kwa kocha mpya, Kim Poulsen.
Katika mchezo huo mashabiki lukuki walionekana kuishaingilia Stars kutokana na kuonesha kila dalili za kuwa na imani ya kocha huyo wakiamini kuwa anaweza kuifikisha mahala pazuri.
Mchezo huo ni kipimo chake cha kwanza Kocha Mkuu Poulsen kabla ya kuivaa Ivory Coast kwenye mechi ya mchujo ya Dombe la Dunia itakayochezwa ugenini Juni 2 mwaka huu.
Kikosi cha Taifa Stars: Juma Kaseja, Shomari Kapombe, Waziri Salum, Aggrey Morris, Kelvin Yondan, Shabani Nditi, Mrisho Ngassa, Frank Damayo, Mbwana Samatta,Haruna Moshi 'Boban', na Mwinyi Kazimoto.
Malawi: Simplex Nthala, Limbikani Mzava, Moses Chavula, Foster Namwera, James Sangala, Joseph Kamwendo/Chimango Kayira, Frank Banda, Dave Banda, Zicco Makanda, RobbinNgalande na Russell Mwafulirwa.
 

Twiga Stars vitani leo
Na Asha Kigundula
TIMU ya Taifa ya soka ya Wanawake ‘Twiga Stars’  leo inashuka dimbani kuvaana na  Ethiopia katika mechi ya kwanza ya raundi ya pili ya michuano ya mchujo kwa ajili ya Fainali za Nane za Kombe la Afrika kwa Wanawake (AWC), mchezo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Addis Ababa, Ethiopia.
Twiga inayonolewa na Kocha Charles Boniface Mkwasa akisaidiwa na Nasra Mohammed, iliondoka jijini Dar es Salaam juzi, huku Kocha wake Mkuu, Mkwasa akijinasibu ya timu hiyo kurejea na ushindi.
Mkwasa alisema kwamba kupitia michezo yao ya kirafiki dhidi ya Zimbabwe na Afrika Kusini ziliwasaidia kwa kiasi kikubwa kujiweka sawa kwa mchezo huo wa leo.
"Tunashukuru pamoja na kufungwa mechi hizo hizo zimetupa changamoto kubwa katika kukiweka sawa kikosi chetu kabla ya mchezo wetu na Ethiopia, ninaamini vijana hawatawaangusha Watanzania,”alisema Mkwasa.
 Timu hizo zitarejeana tena Juni 16 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam iwapo Twiga Stars itafanikiwa kuitoa Ethiopia, itakuwa imepata tiketi ya kwenda kushiriki fainali hizo kwa mara ya pili mfululizo ambapo mwaka huu zitafanyika nchini  Equatorial Guinea Novemba.
Kikosi cha Twiga Stars kilichokwenda Ethiopia,  kinaundwa na  Amina Ally, Asha Rashid (nahodha), Ester Chabruma, Ettoe Mlenzi, Evelyn Sekikubo, Fadhila Hamad, Fatuma Bashiri, Fatuma Khatib, Fatuma Mustafa, Fatuma Omari, Maimuna Said, Mwajuma Abdallah, Mwanahamisi Omari, Mwanaidi Tamba, Mwapewa Mtumwa, Rukia Hamis, Semeni Abeid na Zena Khamis.

No comments:

Post a Comment