- MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Saturday, May 26, 2012

Kova akamata kazi feki za wasanii
Na Charity James
JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limekamata CD 215 za bandia pamoja na mtambo wa kutengenezea kazi hizo za wasanii nchini.

Kamanda wa Polisi wa kanda ya Dar es Salaam, Suleman Kova.
 Kamanda wa Polisi wa kanda hiyo, Suleman Kova, alisema tukio hilo lilitokea Mei 23 mwaka huu maeneo ya Kimara Mavurunza, Dar es Salaam.
Kova, alisema baada ya polisi kupata taarifa za kiintelijensia, walifika eneo la tukio na kufanya upekuzi katika nyumba husika na kufanikiwa kupata CD hizo.
Alisema mbali na kukamata CD hizo walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa Anord Chrispian (26), mwanafunzi wa Chuo cha TRA, ambaye anashikiliwa kwa upelelezi.
Kova, alisema mtuhumiwa alieleza kuwa vitu hivyo ni mali ya kaka yake aitwaye Angelo Kapama, ambaye hakuwepo nyumbani wakati wa ukamataji, na anaendelea kutafutwa kwa ajili ya upelelezi.
cioo

Kalapina: Wasanii chipukizi hawana misingi ya hip hop
Na Hamisi Magendela
KIONGOZI wa kundi la muziki wa kizazi kipya nchini Kalama Masoud 'Kalapina' kutoka 'Kikosi cha Mizinga' amesema chipukizi wengi hawana misingi ya hip hop.
Akizungumza Dar es Salaam juzi, alisema kutokana na sababu hiyo inasababisha wasanii hao kutodumu katika muziki huo na kuwaacha wakonge wakiendelea kutikisa kwenye 'game'.
"Mimi (Kalapina), Sulemani Msindi 'Afande Sele' na wengine wachache ni sehemu ya mfano kutokana na kudumu kwa kipindi kirefu kutokana na kufuata misingi mikuu ya muziki wa hip hop," alisema Kalapina
Kalapina, akiwa katika pozi
Hivyo aliwataka wasanii wachanga kufuata misingi hiyo ikiwemo kuishi na watu vizuri bila ya kujisikia baada ya kutoa 'singo' moja na kufanya vyema katika tasnia ya muziki huo.
Alisema wapo baadhi ya wasanii ambao wanafanya vizuri na wimbo na kujiona mabingwa na kudharau wengine wakati wapo wanaojua zaidi yao.
Kalapina aliongeza kuwa wakati wasanii hao wakijivuna na kujiona mabingwa ukiangalia katika albamu ya nyimbo 10 wimbo mmoja tu ni mzuri.
Hivyo aliwataka wasanii wa aina hiyo kuachana na tabia ambayo inavunja misingi ya muziki huo na ni vyema wakasimamia taratibu zinazotakiwa ili kuifikisha hip hop inapotakiwa.

No comments:

Post a Comment