- MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Saturday, May 26, 2012

Steve Nyerere ahaidi kusomesha watoto wawili yatima

Na Hamisi Magendela
MSANII wa filamu nchini Steve Mengele 'Steve Nyerere' ametoa msaada wa vitu mbalimbali vyenye thamani ya sh mil 3 katika kituo cha kulelea watoto yatima cha Maunga kilichopo Kinondoni Hananasifu Dar es Salaam.
Pamoja na hilo ameahidi kusomesha watoto wawili wa kituo hicho wa kike na wa kiume kuanzia darasa la kwanza hadi la saba kuanzia mwakani.
Steve Nyerere aliyasema hayo wakati wa kutoa msaada huo juzi na kuongeza kuwa aliamua kufanya hivyo kutokana kwa kukamilika kwa filamu yake inayoitwa Mwalimu Nyerere ambayo inasambazwa na Steps Entertaiment.
"Nashukuru nimetimiza nadhiri yangu ya kusaidia watoto yatima baada ya kukamilisha filamu yangu ya Mwalimu Nyerere ambayo nimeirekodia Butiama mkoani Mara na jana imeingizwa sokoni katika maduka mbalimbali nchini," alisema Steve Nyerere.
Msanii wa filamu nchini Steve Mengele Steve Nyerere akikabidhi msaada wa vyakula katika kituo cha watoto Yatima cha Maunga kilichopo Kinondoni Dar es Salaam Mey 24, mwaka huu.
Alisema Baba wa Taifa alikuwa akipenda jamii mbalimbali wakiwemo yatima na kufanya atakuwa ameenzi mambo mazuri ambayo yanastahili kuigwa na wasanii wengine.
Steve Nyerere alisema filamu hiyo imetumia zaidi ya shilingi mil 25 na hadi kukamilika kwake ilitumia miezi mitatu tofauti na filamu nyingine zinazochukua wiki mbili au tatu kukamilika kwake.
Vifaa alivyotoa katika kituo hicho ni pamoja na Sabuni, Mchele,
Unga Maharagwe pamoja na Chandarua.
Pia mlezi wa kituo hicho Zainab Maulid alishukuru kwa msaada huo na kuowambo watu wengine kujitokeza kufanya hivyo ili kusaidia watoto 30 waliopo hapo na wengine 20 wanaolelewa
kwenye familia zao.
Zainab alisema kuwa kituo hicho kinakabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo uhaba wa chakula, magodoro, sare kwa wanafunzi.

cuopp


Yanga mikononi mwa Kifukwe
- Kamati ya Usajili yaomba muongozo TFF
- Jangwani watamba kufanya usajili wa hatari
Na Asha Kigundula
MWENYEKITI wa zamani wa klabu ya Yanga, Francis Kifukwe, anatarajiwa kukabidhiwa timu baada juzi, Mwenyekiti wa Klabu hiyo, Lloyd Nchunga kuachia ngazi.
Nchunga alifikia uamuzi huo baada ya wajumbe wake wanane wa Kamati ya Utendaji kujiuzulu kutokana mgogoro ulioibuka baina yao na Baraza la Wazee wa klabu hiyo.
Wajumbe waliojiuzulu katika kamati hiyo ni Mzee Yusuf, Ally Mayai, Ahmed Seif, Davis Mosha, Patrick, Theonest Rutashoburwa (marehemu) na Mohamed Bhinda na .
Akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu wa Baraza la Wazee, Ibrahim Akilimali, alisema baada ya Nchunga kujiuzulu, timu hiyo atakabidhiwa Kifukwe na wajumbe wenzake wa Bodi ya Wadhamini wa klabu hiyo.
Akilimali, alisema baada ya Nchunga kuchukua uamuzi huo, amewataka wanachama kutulia katika kipichi hiki kifupi ambacho wanahitaji ushirikiano wao.
"Tunampongeza Nchunga kwa ujasiri alioonesha wa kujiuzulu, na licha ya kuwa na mgogoro na yote aliyoyasababisha katika klabu yetu, bado tutaendelea kumtambua kama mwanachama wa Yanga," alisema Akilimali.
Alisema mikakati inayofuata ni kuijenga Yanga, ambapo wanataraji kufanya usajili wa wachezaji ili timu hiyo, iweze kutisha kama Mabingwa wa Ligi ya England Macherster City, TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Real Madrid  na Barcelona za Hispania.
Alisema usajili watakaoufanya utakuwa ni tishio kwani wamedhamiriwa kutetea ubingwa wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika Mashariki na Kati (Kagame Cup).
Akilimali alisema wanatarajia kufanya usajili kwa umakini ingawa tayari wameanza kusajili kimya kimya, lakini wataanika kikosi chao baada ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), kuwapa mwongozo kutokana na kujiuzulu kwa viongozi wao.
Wakati huo huo, Mwenyekiti wa Vijana wa klabu hiyo, Bakil Makele alisema wanasubiri mwongozo kutoka TFF, baada ya Kamati ya Uchaguzi ya Yanga, kuwasilisha barua kwa shirikisho ikitaka kupata maelezo baada ya viongozi wao kujiuzulu.
Na wakati wakisubiri hilo, Kamati ya Sheria Maadili na Hadhi za Wachezaji ya TFF ilikutana jana jioni, inatakiwa kutoa muongoza baada ya kikao hicho juu ya hali iliyopo katika klabu ya Yanga.
Akizungumza Dar es salaam jana, Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura, alisema wamepokea barua kutoka kwa Kamati ya Uchaguzi ya Yanga kuwa wajumbe kadhaa wa Kamati ya Utendaji ya Yanga, akiwemo Mwenyekiti Lloyd Nchunga wamejiuzulu, na inahitaji muongozo.

Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji chini ya Mwenyekiti wake, Alex Mgongolwa, imekutana jana na leo inatarajiwa kutoa muongozo huo kwa Yanga.
 ciooo

Makalla, Zitto kuisapoti Simba Dar Live
Na Asha Kigundula
NAIBU Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makala, ndiye mgeni rasmi wa sherehe za ubingwa wa klabu ya Simba zitakazofanyika Jumapili kwenye Ukumbi wa Dar Live uliopo Mbagara Dar es Salaam.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geofrey Nyange 'Kaburu', alisema licha kuwepo mgeni huyo ambaye atatoa zawadi mbalimbali kwa wachezaji, kutakuwa na viongozi wengine wa kitaifa.
Kaburu alisema viongozi wengine ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta na wengineo wengi.
Kaburu, alisema sherehe hizo zitaanzia Makao Makuu saa 4,asubuhi hadi 6 mchana, baada ya hapo wachezaji, viongozi na benchi la ufundi, watapanda gari la wazi ambapo kutakuwa na kombe litakalotembezwa kwenye matawi mbalimbali na mashabiki kupata fulsa ya kupiga picha na taji hilo.
Alisema baada ya kutoka Msimbazi msafala huo utaelekea Magomeni kwenye Tawi la Mpira Pesa, Ubungo kituo kikuu cha mabasi yaendayo mikoani, wataunganisha barabara ya Mandela kuelekea Buguruni, Karume, Chang’ombe, Uwanja wa Taifa, Kilwa Road, Tandika na kutua Dar Live majira ya saa 10 jioni ambapo sherehe hizo zitaanza rasmi.
Karubu alisema katika sherehe hizo, wachezaji wote watapewa medali na kutangaza wachezaji waliyofanya vizuri katika msimu uliyopita na kutoa tuzo kwa wachezaji hao pamoja n marehemu Patrick Mafisango  kama kuhenzi kwa mchango wake katika msimu huo.
"Tutatoa medali mbalimbali kwa wachezaji wa Simba waliyofanya vizuri katika msimu huo pamoja na marehemu Mafisango, ambaye alichangia kwa kiasi kikubwa kufika tulipofika," alisema Kaburu.
Kiingilio katika Sherehe hizo itakuwa Sh, 5,000 na kwa upande wa viti vya V.I.P Sh, 20,000, kwa upande wa burudani kutakua na Isha Mashauzi, Msondo, Young D na vikundi mbalimbali vya ngoma

No comments:

Post a Comment