Na Eben-Ezery Mende
MWANAMUZIKI nyota wa muziki wa dansi nchini, Rogart Hegga maarufu kwa jina la Caterpillar, yuko mbioni kukamilisha kazi ya kurekodi albamu yake binafsi atakayoitoa kwa mtindo wa 'zing-zong' ambayo tayari amerekodi vibao viwili vya kukata na shoka vinavyotarajiwa kutamba kwa sana vitakaporushwa redioni.
Akizungumza na Jambo Leo jana, Hegga ambaye kwa sasa ni mwanamuziki wa bendi ya Extra Bongo, amesema kuwa ameamua kurekodi albamu pembeni ya bendi ili kujiongezea kipato ambapo pia itamsaidia kurudisha 'makali' yake kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.
![]() |
Rogart Hegga 'Caterpillar'. |
Hegga alisema kuwa, ameweka vionjo mbalimbali katika nyimbo hizo ili kuongeza ladha ambapo zote mbili ameziimba pekee na kuzirekodi katika studio ya On Time Production huku akizipamba kwa mseto wa mirindimo ya rhumba na asili.
Alisema anafuata nyayo za mwanamuziki, Dogo Rama wa bendi ya African Stars 'Twanga Pepeta' anayetesa sasa ambaye naye ametoa albamu yake inayoitwa KM 10,000 inayogombewa sokoni.
No comments:
Post a Comment