Mapro waiumiza kichwa Yanga - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Wednesday, May 29, 2013

Mapro waiumiza kichwa Yanga


Na Mwandishi Wetu
KAMATI ya Usajili ya Klabu ya Yanga, imeanza kuumizwa kichwa katika kuchagua jina moja kati ya wachezaji wake watatu wa kimataifa, Hamis Kiiza, Yaw Berko na Kabange Twite kwa ajili msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara na michuano mbalimbali itakayoshiriki.
Habari kutoka ndani ya Kamati ya usajili ya Yanga zinasema kuwa kati yawachezaji hao inatakiwa asajiliwe mmoja huku wakitambua umuhimu wa kila mmoja.
Chanzo ndani ya kamati hiyo kimesema kwa ujumla wamechanganyikiwa hawajui wafanyeje ili wamsajili atakayewafaa.
"Kwa ujumla hatujui tutafanyaje maana wote kwetu muhimu na jina linalotakiwa ni moja kati ya hao watatu, tunamuhitaji kipa wetu kwa kuutambua mchango wake na hata Kiiza na Kabange," alisema Mjumbe huyo.
Pia mjumbe huyo alisema kuwa klabu yao inaendelea na usajili kwa ajili ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati itakayoanza kutimua vumbi Juni 18 mwaka huu mjini Juba Sudan.
Alisema kuwa mpaka sasa wamewasajili wachezaji wawili tu, ambao ni Mrisho Ngassa na Haruna Niyonzima.
Alisema usajili unaendelea ikiwa ni baada ya kuangalia taarifa ya kocha nafasi gani anazotaka na si kuchukua wachezaji ambao baadae itakuwa tatizo.
Mwisho

No comments:

Post a Comment