Kilichomuua Mangwea chatajwa - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Wednesday, May 29, 2013

Kilichomuua Mangwea chatajwa




JOHANNESBURG, Afrika Kusini
HATIMAYE chanzo kilichosababisha kifo cha rapa,Albert Mangwair aliyefariki ghafla juzi nchini Afrika Kusini kimefahamika.
Ripoti kutoka Hospitali ya  Helen Joseph ya mjini Johannesburg, Afrika
Kusini iliyotolewa na Dk. Shirley Radcliffe  imethibitisha kuwa Albert
Mangwair  amekufa kutokana na kunywa pombe kupita kiasi, mwili
kuchoka na kuzidisha dozi ya dawa za kulevya.
Marehemu, Mangwair
Imeelezwa kuwa Albert (28), alipoteza fahamu akiwa nyumbani kwa rafiki
zake, sampuli ya damu iliyopimwa imeonesha kuwa alikuwa amezidisha
pombe mara tano ya kiasi kinachoruhusiwa kisheria nchini Afrika Kusini
(416mg).
Inadaiwa polisi walikuta chupa mbili tupu za pombe kali aina ya vodka
ndani ya gari waliyotumia.
Taarifa hiyo imebainisha kuwa nyota huyo alikuwa na matatizo ya
kutokula kwa mpangilio (Bulimiafor) kwa miezi kadhaa kabla ya kifo chake
na mwili wake kujawa na uchovu kutokana na kujikita kwenye kumbi mbalimbali za burudani bila ya kupata muda mfupi au  kutopumzika.
Imeelezwa kuwa  sampuli zilizochukuliwa tumboni mwake zilionesha
kuwa marehemu kabla alizidisha dozi mseto ya dawa za kulevya aina ya
heroin, cocaine 'crack'  na bangi  kipimo cha 0.08gms ilikutwa kwenye
damu yake.
Pia ripoti hiyo imebainisha kuwa pia kifo chake kimechangiwa na matatizo
ya moyo na kushindwa kupumua vizuri kitu kilichofuatiwa na kusimama
moyo ghafla na kusababisha kifo chake muda mfupi baadaye!

No comments:

Post a Comment