Majonzi! Mkurugenzi wa Bendi ya Extra Bongo ‘Wazee wa Kizigo’, Ali Choki amepata pigo kubwa la kufiwa na mkewe, Shuea Hamis ‘Mama Shuu’ baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Aliyekuwa mke wa Mkurugenzi wa Bendi ya Extra Bongo ‘Wazee wa Kizigo’, Ali Choki, marehemu Shuea Hamis ‘Mama Shuu’. Akizungumza na Ijumaa Wikienda kwa masikitiko, Choki alisema kwamba mke wake ameugua kwa muda wa miezi tisa akisumbuliwa na tatizo la mguu.
Alisema kwamba katika jitihada za matibabu, mkewe huyo alitibiwa nchini India ikashindikana, akarudishwa nyumbani mpaka mauti yalipomfika usiku wa kuamkia Jumamosi iliyopita.
“Kweli alikuwa akipata mateso makubwa kwani alikuwa hatembei analala tu ndani hivyo kutoa nafasi kwa magonjwa mengine kumshambulia.
“Ukweli nimeumia kwani alikuwa ni mshauri wangu mkuu na ndiye alikuwa kila kitu kwangu
No comments:
Post a Comment