Mwandishi Wetu
MPAMBANO wa mchezo wa masumbwi mkali utakaokutanisha mabondia mbalimbali kutoka kila kona ya Tanzania utafanyika
October 25 katika ukumbi wa friends Corner manzese jijini Dar es salaam akizingumza na waandishi wa habari mratibu wa mpambano huo kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila ‘Super D’
amesema kuwa siku hiyo kutakuwa na mpambano wa mahasimu katika mchezo wa ngumi kati ya bondia Saidi Mbelwa ‘Moto wa Gesi’ na George Dimos mpambano mwingine utawakutanisha Amani Bariki ‘Manny Chuga’ na Ally Bugingo mpambano unaosubiliwa kwa hamu kila kona ya jiji la Dar es salaam ambapo mabondia hawo wamejizolea umaarufu mkubwa kupitia mchezo huo
pambano jingine ni kati ya Juma Fundi atakaezichapa na Hamza Mchanjo wakati Hasani Mandula ataonyeshana kazi na Mohamedi Jaka na Shabani Kaoneka atazipiga na Ibrahimu Maokola anaejiandaa kuwania kucheza ubingwa wa taifa mwishoni mwa mwaka huu Fadhili Boika atazipiga na Godfrey Silver na Habibu Pengo atazidunda na Abdallah Luanje, Kashinde Mohamedi atazidunda na Mohamed Kibaga wakati Sadiki Nuru atakumbana na Mohamed Mbishi
katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na ulinzi wa kutosha kabisa kutokana na kujipanga vizuri katika swala hilo kingilio ni shilingi, 5000; kwa kila mtu mchezo huu utapambwa na burudani mbalimbali.
siku hiyo pia kutakuwa
zikiuzwa DVD mpya za masumbwi ambazo zinaonesha mafunzo mbalimbali ya
mchezo wa ngumi yanavyoanza hatua kwa hatua mpaka kujua kitu kamili katika
mchezo huo pia kunakuwa na mapambano ya mabondia mabigwa wa dunia wa mchezo huo kama Floyd
Maywether, Manny Paquaio,mike Tyson, Mohamed Alli pamoja na mabambano ya ngumi ya ndani
TAARIFA YA KAMATI YA UTENDAJI YA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA ILIYOKUTANA OKTOBA 11, 2014- DAR ES SALAAM
Rais wa TFF, Jamal Malinzi
Kikao cha dharura cha Kamati ya
Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kimefanyika leo
kujadili matukio ya hivi karibuni, hasa mwenendo wa wadau wa Bodi ya
Ligi. Shirikisho linatoa tamko kwa umma kama ifuatavyo:
- Kamati ya Utendaaji imesikitishwa na taarifa za upotoshaji kuhusu kanuni mpya za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), hivyo inaomba radhi kwa wadau ambao wameguswa na kusumbuliwa na matukio hayo.
2.Kufuatia matukio hayo,
Sekretarieti ya TFF kwa niaba ya Kamati ya Utendaji, imefungua mashtaka
kwenye Kamati ya Nidhamu dhidi ya Dk. Damas Ndumbaro ambaye ni mjumbe wa
Bodi ya Ligi na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Klabu ya Simba. Pia
wadau wote waliohusika na upotoshaji huo wakiwemo wafanyakazi wa TFF na
Bodi ya Ligi watashughulikiwa kulingana na nafasi zao.
3.Kutokana na madai ya klabu
kuhusu vipengele kadhaa vya Kanuni za Ligi Kuu 2014/15, Kamati ya
Utendaji imepanga kukutana na viongozi wa klabu za Ligi Kuu siku ya
Jumamosi, Oktoba 18 mwaka huu ili kuwasikiliza na kushauriana kuhusu
changamoto za kikanuni na uendeshaji wa mashindano kwa ujumla.
4.Kamati ya Utendaji itaendelea
kuboresha Kanuni za Uendeshaji Bodi ya Ligi (Governing Regulations) ili
kuweka uwiano wa utendaji na kuepusha tofauti kati ya Bodi ya Ligi,
vilabu na TFF. Aidha Kamati ya Utendaji itafanya kila linalowezekana
kuboresha ligi kwa kuijengea uwezo Bodi ya Ligi kwa lengo la kuwa na
ligi zinazoendeshwa kisasa (Professional Leagues).
KAMATI YA NIDHAMU KUTETA NA WAANDISHI
Mjumbe wa kamati, Kitwana Manara (kushoto)
Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) leo (Oktoba 11 mwaka huu) imesikiliza
malalamiko yaliyowasilishwa mbele yake dhidi ya Dk. Damas Ndumbaro.
Shauri hilo limesikilizwa na
wajumbe wa Kamati hiyo chini ya Makamu Mwenyekiti wake Wakili Jerome
Msemwa. Wajumbe wengine wa kamati hiyo waliosikiliza shauri hilo
lililowasilishwa na TFF ni Kitwana Manara, Kassim Dau na Nassoro Duduma.
Hivyo, Kamati hiyo itakuwa na
mkutano na waandishi wa habari kutangaza uamuzi wake juu ya shauri hilo.
Mkutano huo utafanyika Jumatatu (Oktoba 13 mwaka huu) saa 8 mchana
kwenye ofisi za TFF, Jengo la PPF Tower.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
No comments:
Post a Comment