Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara wa Benki ya NBC ,Bw. Elvis Ndunguru(Kushoto), Akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya KANU EQUIPMENTS, Bw. Warren Heger(Kulia) kwenye hafla ya utiaji saini mkataba wa makubaliano ya kutoa mikopo nafuu kwa wakulima kwa ajili ya kununulia pembejeo za kilimo ili kuongeza tija na ufanisi katika sekta ya kilimo nchini.
Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwakushirikiana na KANU EQUIPMENT jana wametia saini mkataba wa maridhiano ili kutoa mikopo nafuu kwa wakulima kwa ajili ya kununulia pembejo za kilimo ili kuongeza tija na ufanisi katika sekta ya kilimo nchini.
Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika katika Makao Makuu ya Benki ya NBC, Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara Elvis Nduguru alisema; “Sisi Benki ya NBC tukiwa wadau wakubwa wa kilimo nchini tunathamini na kutambua mchango wa kilimo katika pato la taifa. Kilimo kinachangia zaidi ya asilimia 65% ya uzalishaji nchini na pia kinatoa zaidi asilimia 75% ya ajira zote.
Kilimo
ndio uti wa mgongo wa taifa letu. Hivi karibuni Serikali kupitia Waziri
wa Kilimo imetangaza mpango maalum wa kuboresha kilimo ujulikanao kama
“ajenda 10/30” ambao unalenga kuongeza ukuaji wa sekta ya kilimo kutoka
asilia 5 mpaka 10 ifikapo mwaka 2030. Sisi Benki ya NBC tukiwa wadau
wakubwa wa kilimo nchini, tumeona ni vema kuunga mkono juhudi hizi za
Serkali yetu kwa kukutana na wenzetu wa KANU, ambao ni watalaam katika
masuala ya uuzaji wa vifaa vya kilimo kutoa mikopo nafuu ili kuongeza
ufanisi katika uzalishaji. Kupitia maridhiano haya, wanunuzi wa pembejeo
za kilimo kupitia kampuni ya KANU nchi nzima, ikiwemo matrekta,
wataweza kupata mikopo nafuu na ya haraka kununua vifaa kama matrekta
ndani ya siku kumi na nne” alisema.
Awali Mkuu wa Kitengo cha
Kilimo wa Benki hiyo Raymond Urassa akifafanua kuhusu faida na vigezo
kwa wakulima kupitia bidhaa hii alisema; “makubaliano haya tunayosaini
leo yatawawezesha wakulima na wafanyabiashara waliopo kwenye mnyororo wa
thamani wa mazao ya kilimo, kupata zana za kilimo na pembejeo kwa
gharama nafuu na kwa wakati stahiki. Lengo letu ni kuhakikisha Mkulima
anapata trekta lake ndani ya siku kumi na nne huku wakiwa na muda rafiki
wa marejesho ya mkopo kulingana na msimu wa zao husika” alisema.

Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara wa Benki ya NBC ,Bw. Elvis Ndunguru(Kushoto), Akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya KANU EQUIPMENTS, Bw. Warren Heger(Kulia) wakikabidhiana mikataba iliyosainiwa.

Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara wa Benki ya NBC ,Bw. Elvis Ndunguru (Kushoto), Akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya KANU EQUIPMENTS, Bw. Warren Heger (Kulia) wakikabidhiana mikataba iliiyosainiwa huku wadau wengine wakiwa pembeni yao wakishuhudia makabidhiano hayo.

Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara wa Benki ya NBC ,Bw. Elvis Ndunguru wa pili (Kushoto), Akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya KANU EQUIPMENTS, Bw. Warren Heger wa kwanza (Kulia), pamoja na wadau wengine wawili wakizungumza jambo kwa pamoja.
No comments:
Post a Comment