Wataalam
wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu kutoka nchini Korea ya Kusini wanaendesha
mafunzo ya wiki mbili kwa watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu ya
Tanzania (NBS) yenye lengo la kujenga uwezo watumishi hao katika
kuchakata taarifa mbalimbali zikiwemo za kiuchumi.
Akieleza
kuhusu mafunzo hayo jijini Dodoma Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi kutoka
NBS Bw. Daniel Masolwa amesema kuwa mafunzo hayo ni matokeo ya
ushirikiano kati ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu NBS na Ofisi ya Taifa ya
Takwimu ya nchini Korea ya Kusini.
" Mafunzo haya yatawezesha
watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu kuongeza weledi katika
utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku ", alisisitiza Masolwa.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Takwimu nchini Korea ya
Kusini Bw. Charlse Seo amesema kuwa Tanzania ni moja ya nchi
zinazofanya vizuri katika ukusanyaji na uchakataji wa taarifa
mbalimbali ikiwemo za kiuchumi.
"Ushirikiano kati ya Ofisi ya
Taifa ya Takwimu ya Korea ya Kusini na Ofisi ya Taifa ya Takwimu
Tanzania (NBS) umejikita katika mafunzo ya kujenga uwezo na kutoa vifaa
kwa NBS, aidha, mafunzo haya ni natokeo ya ushirikiano mzuri kati
yetu", Alisisitiza Bw. Seo
Kwa upande wake Mratibu wa Mradi wa
ushirikiano kati ya NBS na Ofisi ya Takwimu ya nchini Korea ya Kusini
Bw. Deogratius Malamsha amesema mradi huo ni wa miaka mitatu na ulianza
mwaka 2021 na utakamilika 2023.
Watumishi 15 wa NBS wanashiriki mafunzo hayo ya wiki mbili yanayofanyika Dodoma.
Aidha,
mradi huo unahusisha mafunzo na utoaji wa vifaa ambapo sehemu ya
mafunzo yanafanyika Tanzania na mengine Korea ya Kusini.
Mafunzo
hayo ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa ushirikiano kupitia Ofisi ya
Taifa ya Takwimu na Serikali ya Korea kupitia Ofisi ya Taifa ya Takwimu
ya Korea Kusini.
Thursday, September 22, 2022
New
Korea ya Kusini Yawanoa Watakwimu NBS
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment